Mfanyabiashara Mbutusyo Mwakihaba (40) amefikishwa katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kosa la kusambaza taarifa za uongo
kwamba amemuona Kachero karibu na Hospitali aliyolazwa Mbunge wa Singida
Mashariki, Tundu Lissu.
Mshtakiwa huyo alisomewa kosa lake mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa na Wakili wa Serikali, Janeth Magoho.
Wakili huyo wa Serikali alidai kuwa September 11, 2017 huko Dar es
Salaam kupitia mfumo wa kompyuta alisambaza taarifa hiyo kwenye mtandao
wa kijamii wa WhatsApp.
Mshtakiwa huyo anadaiwa kusema “Huyo ni Kachero wa Usalama wa Taifa
anatambulika kwa jina la Jose ameonekana Nairobi karibu na Hospitali
aliyolazwa Mbunge wa Singida Mashariki, Mh Tundu Lissu mwacheni
mwenzenu.”
Wakili huyo wa Serikali, Magoho alidai kuwa mshtakiwa aliyatoa maneno
hayo kwa nia ya kupotosha umma ambapo baada ya kusomewa shtaka hilo,
mshtakiwa alikana na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi bado
haujakamilika.
Hakimu Nongwa alimtaka mshtakiwa huyo kuwa na wadhamini wawili
wanaoaminika ambao kila mmoja anatakiwa kusaini bondi ya Tsh Milioni 5
ambapo kesi imeahirishwa hadi October 12, 2017 kwa ajili ya kutajwa na
mshtakiwa ameshindwa kukamilisha masharti hayo ya dhamana na kupelekwa
rumande.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Thursday, September 28, 2017
Aliyetoa taarifa za ‘Kachero’ alikolazwa Lissu afikishwa Mahakamani
Tags
KIMATAIFA#
Share This
About kilole mzee
KIMATAIFA
Labels:
KIMATAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment