KAMANDA
wa Kikosi cha Usama Barabarani, Fortunatus Musilimu amezifuta leseni
za madereva saba ambao walikamatwa kwa makosa mbalimbali yakiwemo
kuendesha kwa mwendokasi, kukiuka sheria za barabarani na kusababisha
ajali, vifo na majeruhi.
Akizungumza
na wanahabari jijini Dar es Salaam leo Septemba 28, 2017, Kamanda
Msilimu amesema Jeshi hilo kwa kufuata maagizo ya Rais John Magufuli
limeamua kufanya oparesheni kali usiku na mchana kuwabaini, kuwakamata
na kuwachukulia hatua ikiwemo kuwafungia leseni madereva wote wanaokiuka
sheria za usalama barabarani lengo ikiwa ni kupunguza ajali na vifo
ambavyo vimekuwa vikitokana na ajali hizo.
“Watu
wamezoea oparesheni zetu mchana, kwa sasa tunafanya hadi usiku kwa
maana tochi zetu zinakamata muda wowote, kwa hiyo sisi tutapambana nao
muda wote. Tumeanza na Dumira na sasa tunaendesha oparesheni hii mikoa
yote na barabara zote nchini.
“Kwa
kipindi cha wiki moja ambacho oparesheni imeanza tarehe 14-18, Septemba
2017, tumekamata jumla ya makosa 53,870, tumekamata madereva saba wa
mabasi makubwa yakiwa yanaendehswa kwa mwendo mkali wa Kilometa 90 kwa
saa tena usiku. Baada ya kukamatwa tuliwapeleka mahakamani na wakakiri
makosa yao. Kwa mujibu wa sheria ninatangaza kuwafutia leseni zao wote.
“Taarifa
zao tumezipeleka TRA, SUMATRA na kwa wamiliki wa mabasi (TABOA), iwapo
watahitaji kuendelea na kazi hiyo, watatakiwa kukaa kwa miezi sita kisha
warudi darasani wakasome, wakifaulu waje tuwatahini hadi tujiridhishe
kuwa wameiva ndipo tuwarejeshee madaraja yao ya leseni,” alisema
Musilimu.
Madereva
waliofutiwa leseni zao ni Hamad Shabani Salum (leseni namba
4001852854), Kija Aloyse Mayenga (leseni namba 4001518000), Isack John
Mbijina (leseni namba 4000220395), Hassan Abbas Semazua (leseni namba
4001522366), Stanley Joseph Mosha (leseni namba 4000369436), Abdallah
Hussein (leseni namba 4000482412) na Sempunda Yusuph (leseni namba
119808006515226).
Post Top Ad
Your Ad Spot
Thursday, September 28, 2017
Breaking : LESENI ZA MADEREVA ZAFUTWA
Tags
KITAIFA#
Share This
About kilole mzee
KITAIFA
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment