Kiongozi wa Muungano wa Upinzani nchini Kenya (Nasa) Raila Odinga,
ameilaumu Ikulu ya Nairobi ya State House, kwa kuwazuia vigogo wa
muungano huo, Kalonzo Musyoka na Moses Wetangula kusafiri kwenda nchini
Uganda.
Bw. Odinga amesema kuwa viongozi hao wawili walizuiwa kwenye uwanja wa
kimataifa wa Jomo Kenyatta walipokuwa wakiondoka kwenda nchini Uganda
ambapo Bw. Musyoka angekuwa ahutubie mkutano wa sherehe za kufuzu.
Musyoka alikuwa akielekea kwenye chuo cha Uganda Technology and Management ambapo yeye ni chansela.
Licha ya wawili hao kuruhusiwa kuondoka, Bw. Odinga alisema kuwa hiyo
isharaya kuzoroteka kwa haraka kwa hali ya kisiasa nchini na mikakati ya
kujaribu kuzua hofu nchini.
Kupitia taarifa Bw. Odinga alisema kuwa polisi waliwaambia wawili hao
kuwa viongozi wote wa upinzani watahitaji ruhusa kutoka Ikulu ya Nairobi
kabla ya kuondoka ndani ya nchi.
"Nasa inalaani jihada za hivi punde ya kuingilia uhuru na kuwahangaisha viongozi wake wakuu," taarifa hiyo ilisema.
Alisema kuwa upinzani utapuuza agizo lolote kwa kuwa viongozi wake hawahitaji ruhusa yoyote ya kusafiri nje ya nchi.
"Upinzani nchini Kenya ni lazima uwe huru kama sehemu ya siasa za Kenya
na ni lazima uruhusiwe kuendelea na mikakati yake kama serikali mbadala
na sauti ya watu kwa mujibu wa katiba, kwa mujibu wa katiba." Odinga
alisema.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Thursday, September 28, 2017
Viongozi wa upinzani wazuiwa kwenye uwanja wa ndege Nairobi
Tags
KIMATAIFA#
Share This
About kilole mzee
KIMATAIFA
Labels:
KIMATAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment