Na Yusuph Mlandula
Taasisi
ya The Desk & Chair Foundation (TD&CF) Tawi la Tanzania
imekabidhi kisima cha maji, ndoo na vikombe vya kuchotea maji kwa Shule
za Msingi Nyamagana A na B za Jiji la Mwanza.
Hafla
ya kukabidhi kisima hicho pamoja na ndoo 24 na vikombe vilivyogharimu
zaidi ya shilingi milioni 4.5, ilifanyika mwanzoni mwa juma hili
ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Meya wa Jiji la Mwanza ambaye pia ni
Diwani wa Kata ya Nyamagana (CCM) Bw. Bhiku Kotecha.
Akizungumza
kabla ya kukabidhi kisima hicho, Mwenyekiti wa The Desk & Chair
Foundation Tawi la Tanzania Bw. Sibtain Meghjee alisema kisima hicho
kitazisaidia shule hizo na kuepuka gharama kubwa za malipo ya ankara za
maji na aliuomba uongozi wa shule hizo uhakikishe unakitunza kisima
hicho vizuri ili kidumu.
Alisema
kuwa baadaye taasisi hiyo itaangalia jinsi ya kubadili mfumo unaoweza
kutunzika kikamilifu kwa kuweka tanki la kuhifadhia maji na mota ya
kusukuma maji kutoka kisimani hadi kwenye tenki hilo ili maji yafike
maeneo yote kwa urahisi.
Akizungumza
kwa niaba ya walimu na wanafunzi wa shule hizo, Mwalimu Mkuu wa Shule
ya Msingi Nyamagana B Bw. Anatory Mnono alisema msaada huo umekuja muda
muafaka kwani utawapunguzia mzigo mkubwa uliokuwa umewaelemea.
“Msaada
huu wa kisima umetupunguzia changamoto ya malipo ya maji na kweli
mzigo huu ulituelemea mno.Tutayatumia maji haya kuboresha mazingira ya
shule zetu kwa kupanda miti, kufanya usafi na matumizi mengine ya
kawaida.Tunaishukuru sana Taasisi ya The Desk & Chair, ” alisema.
Bw.
Mnono alieleza kuwa si mara ya kwanza kwa taasisi hiyo kuzisaidia shule
hizo za Nyamagana A na B zenye jumla ya wanafunzi 772 na walimu 27
kwani pia iliwahi kuwajengea matundu 24 ya vyoo kwa matumizi ya walimu
na wanafunzi pamoja na kuwapa madawati zaidi ya 200 na kukarabati
vyumba vya madarasa na madawati yote mabovu.
Naibu
Meya wa Jiji la Mwanza ambaye pia ni Diwania wa Kata ya Nyamagana (CCM)
Bw. Bhiku Kotecha akizindua kisima cha maji kilichokabidhiwa na Taasisi
ya The Desk & Chair Foundation Tawi la Tanzania kwa Shule za Msingi
za Nyamagana A na B mwanzoni mwa juma hili ambapo diwani huyo alikuwa
mgeni rasmi kwenye hafla ya kukabidhi msaada huo.Kulia ni Mwenyekiti wa
Taasisi hiyo Bw. Sibtain Meghjee.
Naibu
Meya wa Jiji la Mwanza ambaye pia ni Diwania wa Kata ya Nyamagana (CCM)
Bw. Bhiku Kotecha akizungumza wakati akizindua kisima cha maji
kilichokabidhiwa na Taasisi ya The Desk & Chair Foundation Tawi la
Tanzania kwa Shule za Msingi za Nyamagana A na B mwanzoni mwa juma hili
ambapo diwani huyo alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya kukabidhi msaada
huo.Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Bw. Sibtain Meghjee.
Naibu
Meya wa Jiji la Mwanza ambaye pia ni Diwania wa Kata ya Nyamagana (CCM)Kata ya Nyamagana (CCM)
Bw. Bhiku Kotecha akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa wanafunzi wa shule za Nyamagana A na B
Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Nyamagana Anatory mnono akizungusha
mkono wa kisima cha maji kulia ni Mwenyekiti wa The Desk & Chair
Sibtain Meghjee, na kushoto ni Naibu Meya wa jiji la Mwanza Bhiku
Kotecha
No comments:
Post a Comment