Abiria
wa Shirika la Ndege la Fastjet wameshindwa kusafiri kwende mkoani mbeya
kutokana na ndege hiyo kushindwa kuruka kwa kukosa kifaa cha kuwasha na
kuzimia ndege katika uwanja wa kimataifa wa Songwe.
blog yetu ilifika katika uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere na
kukuta abiria wakiangaika bila ya kuwa na msaada mbadala wa safari yao
na kuzunguma nao ndipo abiria mmoja aliyejitambulisha kwa jina la
Sylvester Lwila akaamua kueleza kuwa wamekaa hapo uwanjani kuanzia saa
sita na nusu mpaka saa mbili usiku bila ya mafanikio ya Safari.
"nimekuja
hapa uwanjani saa sita tuka Board vizuri tu na kukaa ndani ya ndege kwa
zaidi ya saa moja lakini baadae tukaletewa taarifa kuwa tutoke nje ya
ndege na mizigo yetu ndege imepata itirafu hivyo inafanyiwa matengenezo
kisha baadae tutaingia itaruka ndipo wote tukatoka"anasema Lwila.
anasema
kuwa wamekaa uwanjani hapo kwa zaidi ya saa sita bila mafanikio hivyo
wakamua kuanza kudai nauli zao lakini mmoja wafanyakazi wa shirika hili
akatuambia hawawezi kurudisha nauli leo hivyo wanatupeleka kulala katika
moja ya hoteli iliyopo katika maeneo ya tabata.
hata
hivyo mpaka blog yetu iliondoka uwanjani hapo kulibakia abiria
watatu ambao waligoma kwenda kulala katika hoteli hiyo wakitaka wapewe
pesa zao.
hata
hivyo Mwandishi wetu alifanya jitihada za kumtafuta afisa uhusiano na
Masoko wa Fastjet, Lucy Mbogoro aliweza kuthibitisha kuwa ndege hiyo
imepata itilafu ya kifaa cha kuwasha na kuzimia ingini ya ndege katika kiwanja cha
Songwe mkoani Mbeya hivyo aitaweza kusafiri mpaka siku ya Alhamisi
ambapo kifaa hicho kitakapokuwa kimenunuliwa kutoka nje ya nchi.
amesema
kuwa kwa sasa ni vigumu kutaja lini ndege hiyo itaweza kusafiri kwenda
mbeya hivyo abiria wote waliokata tiketi za awali watarudishiwa na
kuharishiwa safari zao.
Sehemu
ya abiria wa shirika la ndege la Fastjet wakiwa wamekwama na kuduwaa
katika ofsi za Fastjet zilizopo katika uwanja wa ndege wa mwalimu
nyerere jijini Dar es Salaam mara baada ya abiria hao kukwama kushindwa
kusafiri kwenda mbeya kutokana na ndege hiyo waliyotarajia kusafiri nayo kukosa kifaa cha kuwashia na
kuzimia ndege katika uwanja wa kimataifa wa Songwe mkoani Mbeya hali
iliyo walazimu abiria hao kupelekwa kulazwakatika moja ya nyumba za
wageni zilizopo Tabata jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa abiria akiwa ameketi chini akiwa amechoka mara baada ya kupata taarifa kuwa hakuna uhakika wa kusafiri kwenda mbeya na ndege ya Fastjet
Sehemu
ya abiria waliokwama kutokana na kushindwa kusafiri kutokana na ndege
hiyo kukosa kifaa cha kuwasha na kuzimia ndege katika uwanja wa
kimataifa wa Songwe mkoani Mbeya
No comments:
Post a Comment