Februari
2015, Rais wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Kenyatta alimkabidhi Rais mstaafu
wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete nafasi ya Uenyekiti wa Jumuiya
ya Afrika Mashariki katika mkutano wa 16 wa Wakuu wa Jumuiya hiyo Jijini
Nairobi Kenya.
Kutokana
na hali ya mgogoro wa kisiasa katika nchi ya Burundi, ambayo ilipaswa
kukabidhiwa nafasi ya Uenyekiti wa Jumuiya mwaka 2016, Wakuu wa Jumuiya
hiyo waliamua kwa kauli moja kuwa Tanzania kupitia Rais Dkt. Rais John
Pombe Magufuli kuendelea na nafasi hiyo.
Katika
Mkutano wa 18 wa kawaida wa Wakuu wa Jumuiya hiyo uliofanyika Jijini
Dar es Salaam tarehe 20 Mei,2017, Rais Magufuli alisema katika kipindi
cha Uongozi wa Tanzania katika Jumuiya hiyo mafanikio mbalimbali
yalipatikana ikiwemo utekelezaji wa ajenda ya utengamano katika eneo la
ushuru wa forodha linaloshuguhulikia vikwazo vya biashara visivyo na
kodi.
Anasema
katika ushirikiano wa kifedha Tanzania imewezesha kuandwa miswada ya
uanzishwaji wa taasisi ya fedha ya Jumuiya itakayokuwa Taasisi ya mpito
kabla ya kuanzishwa kwa Benki kuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Aidha,
Rais Magufuli alisema mafanikio mengine ni pamoja na ujenzi wa
miundombinu ikiwemo mradi wa ujenzi wa barabara ya Arusha - Holili -
Taveta hadi Voi, na kukamilika kwa upembuzi wa mradi wa barabara ya
Malindi- Lungalunga- Tanga – Bagamoyo.
Aidha
Rais Magufuli alisema pia barabara za Lusahunga- Lusumo- Kigali na
Nyakanazi- Kasulu- Rumonge –Bujumbura ziko kwenye hatua mbalimbali za
usanifu, ikiwa ni sambamba na ujenzi wa vituo vya ukaguzi mipakani,
ambapo vituo 9 kati ya 15 tayari vimeanza kufanya kazi.
Katika
masuala ya amani na usalama, Rais Magufuli alisema kuwa zimefanyika
jitihada mbalimbali zinazosaidia kupunguza uhasama miongoni mwa pande
zinazokinzana hususani katika nchi za Burundi na Sudani ya Kusini.
“Nitoe
pongezi za dhati kwa msuluhishi wa mgogoro wa Burundi, Rais Yoweri
Museveni pamoja na mpatanishi wa mgogoro huo Rais Mstaafu wa Tanzania
Benjamin Mkapa wamefanya kazi kubwa sana,” alisema Rais Magufuli.
Rais
Magufuli alizitaka pande zinazokinzana katika nchi zenye migogoro
katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kutanguliza maslahi ya mataifa yao
mbele na kuweka nyuma maslahi binafsi kwa maendeleo ya nchi zao.
Katika
kipindi cha miaka miwili ambacho Tanzania imekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya
hiyo, utawala bora na demokrasia umeimarika kwa ambapo mwaka huu nchi
za Kenya na Rwanda zinatarajia kufanya Uchaguzi Mkuu.
Aidha
katika kipindi hicho pia Jumuiya hiyo imeweza kukuza uhusiano na
ushirikiano na mashirika makubwa ya Kimataif ikiwemo Benki ya Dunia,
Benki ya Maendeleo ya Afrika ambapo Jumuiya imeweza kusaini mkataba wa
fedha wenye thamani ya Dola milioni 300.
“Tumeweza
kupunguza matumizi ndani ya sekretarieti kutoka dola milioni 12.6
zilizotumika kipindi kilichopita hadi kufikia dola milioni 9.1
nampongeza sana Katibu Mkuu WA Jumuiya kwa kubana matumizi hayo”
anasema Rais Magufuli
Kwa
upande wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni ambaye kwa sasa ni
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, amebainisha kuwa ustawi wa maendeleo ya
wananchi , undugu na ulinzi ni masuala kadhaa ambayo hayana budi kupewa
kipaumbele ili ili kuimarisha uhusiano wa nchi za Jumuiya hiyo.
“Tunapozungumza
kuhusu Jumuiya ya Afrika Mashariki, tunazungumzia juu ya ustawi wa
maendeleo yetu, familia yetu, nchi zetu na hata soko letu, hivyo
yatupasa kuzidisha utangamano kwa maendeleo ya Jumuiya,” anasema Rais
Museveni.
Mkutano
huo ulijadili ajenda mbali mbali zikiwemo za namna ya kuwezesha uundaji
wa magari katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kupunguza uagizaji
wa magari yaliyotumika kutoka nje ya Jumuiya.
Ajenda
nyingine ni pamoja na kuzuia ama kuondoa uingizaji wa nguo na viatu vya
mitumba katika nchi wanachama kutoka nje. Aidha Viongozi hao pia
walijadili namna endelevu ya uchangiaji wa bajeti ya Jumuiya hiyo kwa
nchi wanachama.
Akizungumzia
suala la Mkataba wa Ushirikiano wa Kiuchumi (EPA) ambao haukuweza
kusainiwa na Tanzania wakati ikiwa mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Rais
Museveni alisemaViongozi wa Jumuiya hiyo walibaini kasoro kadhaa ambazo
zingeweza kuleta madhara katika sekta za viwanda za nchi hizo.
Aliongeza
kuwa yeye binafsi ataongoza ujumbe wa wa wataalamu kutoka Jumuiya ya
Afrika Mashariki watakaokwenda yaliko makao makuu ya EU ili kujadili
kwa kina juu ya EPA na kufikia ufumbuzi.
Aidha,Jumuiya
ya Afrika Mashariki ni Taasisi ya Kiserikali (inter-Governmental
Organization), iliyoanzishwa na nchi za Tanzania, Kenya na Uganda.
Mkataba ulianzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki ulisainiwa tarehe 30
Novemba, 1999 na ulianza kutumika rasmi mnamo tarehe 7 julai 2000.
Nchi
za Rwanda na Burundi zilijiunga katika Jumuiya ya Afrika Mashariki
mwaka 2007. Jumuiya ya awali ya Afrika ya Mashariki iliundwa mwaka 1967
na kuvunjika mwaka 1977 kulitokana na sababu mbalimbali zikiwemo za
kisiasa, kijamii na kiuchumi.
Ibara
ya 5(1) ya Mkataba wa kuanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki imeainisha
madhumuni ya kuanzisha Jumuiya kuwa ni kupanua na kuimarisha ushirikiano
baina ya nchi wanachama katika nyanja za kisiasa, kiuchumi, kijamii,
kiutamaduni, ulinzi na usalama, sheria na mahakama kwa manufaa ya
wananchi wa nchi wananchama.
Katika
kufikia lengo hilo kuu, Ibara ya 5(1) ya Mkataba wa kuanzisha Jumuiya
ya Afrika Mashariki imeainisha uendeshaji wa mtangamano wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki utafanyika hatua kwa hatua. Hatua hizo zikiwa ni Umoja
wa Forodha, Soko la Pamoja, Umoja wa Fedha na Shirikisho la Kisiasa.
No comments:
Post a Comment