Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro jana Alhamis June 15,2017
amefanya ziara katika kata ya Didia halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Vijijini na kukagua miradi ya maendeleo.
Mbali
na kutembelea miradi hiyo ambayo mradi wa maji wa visima virefu,zahanati
ya Didia na Kituo cha Polisi Didia pia amezungumza na wananchi wa
kijiji cha Chembeli kilichopo katika kata ya Didia.
Matiro
alikuwa ameambatana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya
ya Shinyanga lakini pia watalaam mbalimbali kutoka halmashauri ya
wilaya ya Shinyanga wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri
hiyo,Bakari Kasinyo.
Tazama picha za matukio yaliyojiri wakati wa ziara ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa ziara yake jana Alhamis June 15,2017 katika kata ya Didia halmashauri ya wilaya ya
Shinyanga vijijini ambapo alisisitiza umuhimu wa wananchi kushiriki
katika shughuli za maendeleo.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa ndani ya jengo la Kituo
cha Polisi Didia ambacho kipo mbioni kukamilika ujenzi wake
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisilikiza maelezo kutoka kwa
diwani wa kata ya Didia Luhende Masele ambaye alisema ujenzi wa kituo
hicho unalenga kuwasogezea karibu wananchi huduma za kipolisi ili
kukabiliana na vitendo vya kihalifu katika mji wa Didia ambao una
wafanya biashara wengi
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ambaye ni mwenyekiti wa kamati
ya ulinzi na usalama akiondoka na msafara wake katika kituo cha polisi
Didia kuangalia jinsi ujenzi unavyoendelea
Mkurugenzi
Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini Bakari Kasinyo
akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na msafara wake wakiwa katika
zahanati ya kijiji cha Didia ambayo inaendelea kujengwa
Mkurugenzi
Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini Bakari Kasinyo
(kulia) akielezea jinsi ujenzi wa zahanati ya Didia ulivyokwama
kumalizika kutokana na kukosekana kwa pesa
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na msafara wake wakiondoka katika zahanati ya kijiji cha Didia
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia bomba la maji ya
kisima kirefu katika kijiji cha Chembeli.Mradi upo katika kijiji cha
Didia na Bukumbi lakini kijiji cha Chembeli kimesaidiwa mabomba mawili
kwa ajili ya wananchi hata hivyo changamoto ni kwamba bomba linaloleta
maji limekuwa likipasuka mara kwa mara hivyo kusababisha kero kwa
wananchi
Hapa
ni katika moja ya eneo ambapo bomba la maji limekuwa likipasuka na
wananchi kulazimika kulifunga kwa mapira/kamba za kuvutika.Mkuu wa
wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisikiliza maelezo kwa Mhandisi wa
maji wa halmashauri ya Shinyanga Vijijini Sylivester Mpemba.
Bomba likiwa limefungwa kwa mapira/kamba za kuvutika baada ya kupasuka hivi karibuni
Mhandisi
wa maji wa halmashauri ya Shinyanga Vijijini Sylivester Mpemba
akielezea namna inavyotokea bomba la maji kupasuka. Hata hivyo mkuu wa
wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alimuagiza kufuatilia na kuchukua
hatua madhubuti kuhusu tatizo la bomba la maji kupasuka mara kwa mara
katika kijiji cha Chembeli
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na wananchi wa
kijiji cha Chembeli ambapo aliwataka kutunza mradi wa maji uliopo katika
kijiji hicho sambamba na kuwahamasisha kulima mazao yanayostahili ukame
kama vile mtama,uwele badala ya kutegemea mahindi pekee ili kukabilina
na njaa
Wakazi wa kijiji cha Chembeli wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Mkazi wa kijiji cha Chembeli akielezea kero zilizopo katika kijiji hicho
Mkazi
wa kijiji cha Chembeli Maria Tungu akielezea kero ya maji katika kijiji
hicho ambapo wanawake wanalazimika kusafiri umbali mrefu kufuata huduma
ya maji katika visima na mto unaounganisha kijiji hicho na kijiji jirani
cha Buyubi
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimsikiliza mkazi wa kijiji cha Chembeli wakati akielezea kero yake
Diwani wa kata ya Didia Luhende Masele akizungumza katika kijiji cha Chembeli
Katibu tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi akizungumza katika kijiji cha Chembeli
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini Bakari Kasinyo
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwasili katika kitongoji cha
Danduhu kijiji cha Didia ambapo mkazi wa eneo hilo Mashaka Mayala
Komanya amejenga nyumba juu ya mradi wa maji
Nyumba iliyojengwa juu ya mradi wa maji
Diwani
wa kata ya Didia Luhende Masele akimweleza mkuu wa wilaya hatua
walizozichukua kutokana na mwananchi huyo kujenga nyumba juu ya mradi wa
maji ya visima virefu uliopo katika kata hiyo ikiwa ni kukubaliana
bomba linalopita katika nyumba hiyo lihamishiwe karibu na barabara kwani
halipitishi maji kwa sasa.Masele alisema mwenye nyumba hiyo anadai
mradi huo ulipitishwa hapo bila yeye kushirikishwa
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimuagiza mkurugenzi wa
halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini kuhakikisha taratibu za
vikao zinafuatwa kwa kuandika muhtasari wa makubaliano watakayoyafikia
ili kupata muafaka kuhusu jengo hilo kujengwa juu ya mradi wa maji na
kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji
Mkurugenzi
Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini Bakari Kasinyo
akimpa maelekezo afisa mtendaji wa kijiji cha Didia Shimba Waziri kuhusu nyumba hiyo kujengwa juu ya mradi wa maji.
No comments:
Post a Comment