Mkurugenzi wa Kampuni ya Candy And Candy Bw. Joe Kariuki
akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelelzo
leo wakati akitambulisha Aplication yake mpya kwa ajili ya kuuza Vyakula,
Vinywaji na Filamu Movie leo, kushoto ni Meneja wa kampuni hiyo Bi Hasna
Mwishehe.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Candy And Candy Bw. Joe Kariuki akionyesha Aplication hiyo jinsi
inavyofanya kazi wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa
Idara ya Habari Maelelzo leo wakati akitambulisha Aplication yake mpya kwa
ajili ya kuuza Vyakula, Vinywaji na Filamu Movie leo, kushoto ni Meneja wa
kampuni hiyo Bi Hasna Mwishehe
Mkurugenzi wa
Kampuni ya Candy And Candy Bw. Joe Kariuki akimpigia simu mmoja wa wamiliki wa
mgahawa ulioko Sinza na kuagiza chakula ili aletewe alipo wakati akitambulisha
Aplication yake mpya kwa ajili ya kuuza Vyakula, Vinywaji na Filamu Movie leo,
kushoto ni Meneja wa kampuni hiyo Bi Hasna Mwishehe.
Kwa mara ya kwanza kampuni
ya Candy and Candy imeanzisha Application mpya inayojulikana kama NIKO HUB
ambayo ni mkombozi wa wafanyabiashara wengi na watumiaji wa mtandao huo.NIKO
HUB inajihusisha na mambo yote yanayohusu vyakula,vinywaji na filamu (movies).
Lengo kubwa la NIKO HUB ni
kunyanyua wafanyabiashara wakubwa na wadogo kwa kupanua soko lao na kujiongezea
kipato zaidi zaidi na kumuondolea usumbufu mteja wakati anapohitaji huduma
ambapo Aplication hii inamfanya mteja kuagiza bidhaa na kuletewa mahali alipo
kikubwa anachotakiwa kufanya ni kupakua Aplication hii kwenye Google Play bure
na kisha anaanza kuitumia kwenye simu yake.
NIKO HUB inafanya kazi
mahali popote ulipo katika bara la Afrika na popote unapoenda huhitaji kupakua
Aplication nyingine bali unaendelea kutumia ileile, Aplication hii pia
inabadili lugha kulingana na lugha inayotumika katika nchi husika kwa mfano
Tanzania inapatikana kwa kiswahili lakini ukienda kwenye nchi za kiarabu
zilizoko Afrika itakuletea lugha ya kiarabu na ukienda nchi inayotumia lugha ya
kifaransa itafanya hivyo pia N.K.
Jambo kubwa ni kwamba NIKO
HUB pia imeandaa tamasha litakalojulikana kama NIKO HUB EAT OUT FESTIVAL ambalo
litafanyika siku ya sikukuu ya Eid na hakutakuwa na kiingilio kwa washiriki
ambapo litashirikisha wajasiriamali mbalimbali wanaojihusisha na uuzaji wa
vyakula mbalimbali na vinywaji.
Tamasha hilo litafanyika
jijini Dar es salaam kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni na litajumuisha
burudani mbalimbali huku wasanii kadhaa wakitumbuiza kwenye tamasha hilo.
Tamasha hilo pia kutakuwa
na michezo ya watoto ambapo wazazi na walezi watapata fursa ya kujumuika pamoja
na familiazao .Aidha kutakua na mafunzo mbalimbali kwa ajili ya kuboresha
biashara zao.Kupitia NIKO HUB EAT OUT FESTIVAL huku watoto wakifundishwa kuishi
katika mazingira ya usafi kwa ajili ya afya zao.
Kampuni ya Candy n Candy
iliyoanzishwa rasmi mwaka 2014 chini ya uongozi wa Joe Kariuki, ambayo ni
kampuni Tanzu ya makampuni ya Candy and Candy Records, Candy Air, Candy Mining,
Candy Rhythm Night Club na The evening Post Blog,Baabkubwa pamoja na Big ishu yameingia
kwenye soko na kuleta mageuzi katika biashara.
Kampuni ya Candy Records
imewahi kufanya kazi na wasanii wengi wa ndani na nje ya nchi ya Tanzania
wakiwemo Mr Nice, Baby Madaha, Top C, Fat S,Hussein Machozi na wengine wengi.
No comments:
Post a Comment