Huduma
hiyo ambayo pia inapatikana kote nchini, inajulikana kama "Jamii, Ngao
ya Afya" ambapo itawawezesha wateja wa Vodacom waliojiunga na hudumaya
M-Pesa kupata matibabu kote nchini katika hospitali na vituo vya afya
vilivyoidhinishwa kutoa huduma hiyo.
Huduma
ya matibabu ya Jamii huwawezesha watumiaji wa Vodacom kupata matibabu
kwa gharama nafuu ambapo kwa mwanachama mmoja atalipa shilingi 7,000 kwa
miezi mitatu, miezi sita atalipa shilingi 23,000 na kwa mwaka atalipa
shilingi 44,000 ambapo atanufaika na huduma bora za matibabu.
Ni
rahisi sana kujiunga na huduma ya bima ya afya ya "Jamii" kutoka Vodacom
Tanzania kwa kushirikiana na Jubilee Unsurance, wasiliana na mtoa
huduma kwa wateja kwa kupiga nambari 0743 888 111 ama 0755 88 5515
Diwani
wa Kata yaKirumba, Alex Ngusa, akizungumza jana kwa niaba ya Naibu Meya
wa Jiji la Mwanza kwenye uzinduzi wa Bima ya Afya ya Jamii katika
viwanja vya Igoma Jijini Mwanza.
Asma
Athuman ambaye ni Meneja Mafunzo kutoka Vodacom mkoani Mwanza,
akifafanua jambo kwenye uzinduzi wa Bima ya Afya ya Jamii katika viwanja
vya Igoma Jijini Mwanza.
Asma
Athuman ambaye ni Meneja Mafunzo kutoka Vodacom mkoani Mwanza,
akifafanua jambo kwenye uzinduzi wa Bima ya Afya ya Jamii katika viwanja
vya Igoma Jijini Mwanza.
Wakazi
wa Jiji la Mwanza wakimsikiliza kwa makini, Asma Athuman ambaye ni
Meneja Mafunzo kutoka Vodacom mkoani Mwanza, wakati akifafanua jambo
kwenye uzinduzi wa Bima ya afya ya Jamii katika viwanja vya Igoma Jijini
Mwanza.
Maureen
Ndekana kutoka USAID akizungumzia huduma ya Jamii kwenye uzinduzi wa
Bima ya Afya ya Jamii katika viwanja vya Igoma Jijini Mwanza.
Victoria
Chale ambaye ni Meneja Mauzo na Usambazaji kutoka Vodacom Mwanza
akiwahamasisha wakazi wa Jiji la Mwanza kujiunga na huduma ya afya ya
Jamii-Ngao ya Afya ambapo wananchi wengi walihamasika kujiunga na huduma
hiyo
- Noel Mazoya ambayeni Meneja Masoko, huduma za kifedha kutoka Vodacom Tanzania, akizungumza kwenye uzinduzi wa huduma ya afya ya Jamii-Ngao ya Afya kwenye viwanja wa Igoma Jijini Mwanza
Wakazi wa Jiji la Mwanza wakishuhudia uzinduzi wa huduma ya Jamii-Ngao ya Afya katika viunga vya Igoma Jijini Mwanza jana
Shukurani
za pekee ziwaendee Vodacom Tanzania, Jubilee Insurance, ADGE Point kwa
ufadhili wa watu wa Marekani USAID kwa kuwafikia wakazi wa mkoa wa
Mwanza katika kunufaika na huduma ya Bima ya afya ya Jamii ambapo kwa
mwezi mzima timu ya usajili wa huduma hiyo itazunguka maeneo mbalimbali
ikiwemo minadani ili kuwasajili wananchi wote.
Pia
ahsante kwa 102.5 Lake Fm Mwanza, kwa kujumuika kwenye kuhakikisha
wananchi wote wa Mwanza wanaifahamu huduma hii ya "Jamii-Ngao ya Afya".
Kwa msaada zaidi piga simu nambari 0743 888 111 ama 0755 88 55 15
No comments:
Post a Comment