A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Sunday, September 1, 2024

ORYX GAS TANZANIA YAENDELEA KUWA MKOMBOZI KWA MAMA NA BABA LISHE YATOA MITUNGI NA MAJIKO 1000 MKOA WA MBEYA.

KAMPUNI ya Oryx Gas Tanzania imeendelea kuwa mkombozi kwa Mama na Babalishe baada ya kutoa mitungi na majiko yake 1000 kwa washiriki wa mashindano ya kupika kwa gesi ya Oryx mkoani Mbeya ili kuwawezesha kurahisisha shughuli zao za mapishi huku Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga akieleza Serikali imewataka wadau wa gesi kuangalia uwezakano wa kuwa na gesi ambayo Mwananchi atanunua kidogo kidogo.
Akizungumza wakati akihitimisha mashindano hayo,Naibu Waziri Judith Kapinga aliyekuwa mgeni rasmi amesema Serikali imekuwa mstari wa mbele kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini na lengo ifikapo mwaka 2034 asilimia 80 ya wananchi wawe wanatumia nishati mbadala kupikia.

"Maombi ya wananchi kwa wadau wa gesi ni kupunguzwa kwa bei ya gesi ambayo kwa sasa ni kubwa.Tunashauri wadau katika sekta hii ya  tengenezeni mfumo ambao utakuwa rafiki kwa Mwananchi kununua gesi kidogo kidogo kwa siku badala ya kutoa fedha nyingi kwa wakati mmoja,"amesema.
Amesisitiza kukiwa na uwezo wa gesi kununuliwa kidogo kidogo anaamini wananchi wengi watatumia gesi na hivyo kusaidia kupunguza Kasi ya uharibu wa mazingira lakini pia kulinda afya za wananchi.

Naibu Waziri Kapinga amesema katika mwaka wa fedha uliopita wamegawa mitungi kwa wananchi na mwaka huu wa fedha wametenga fedha kwa ajili ya kuendelea kugawa nishati mbadala ya kupikia kwa wananchi huku akisisitiza kuwa  Rais DK.Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuona asilimia kubwa ya Watanzania wanatumia nishati hiyo.

Kuhusu mashindano hayo ya mapishi , Naibu Waziri Kapinga amempongeza Spika wa Bunge Dk.Tulia Ackson kuandaa mashindano hayo makubwa na kushirikisha Mama na Baba Lishe 1000 kushindana kupika kwa gesi kwani yamekuwa ya mfano na yametumika kutoa elimu ya nishati na utunzaji mazingira.


Ametumia nafasi hiyo kuwashukuru Oryx kwa kuendelea kuishika mkono Serikali katika kusaidia kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia,wanafanya kazi nzuri na wamekuwa wakifika kila mahali wakigawa mitungi na majiko yake kwa jamii.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Oryx  Gas Tanzania Benoit Araman amesema lengo kuu la mashindano ya mapishi ni kuhamasika matumizi ya nishati safi kwa lengo la kulinda mazingira ambayo yamekuwa yakiharibiwa kwasababu ya kukata kuni na mkaa.

"Kwa miaka zaidi ya 15 iliyopita upatikanaji wa nishati ya kupikia umekuwa ukipangwa na kujadiliwa  lakini hivi sasa Serikali inayoongozwa na Rais DK.Samia Suluhu Hassan amekuwa na hamasa kubwa ya kuhimiza wananchi kutumia nishati safi ya kupikia.

"Oryx Gasi tunaamini  kupika kwa gesi kunakwenda kusaidia kulinda mazingira sambamba na kupunguza muda mwingi kwa wanawake kuwa porini kutafuta kuni na mkaa kwa ajili ya kuanda chakula.Pia kupika kwa gesi kutasaidia kuwalinda wanawake dhidi ya wanyama wakali walioko  misitu lakini kuwalinda dhidi ya vitendo vya  ukatilii ambavyo wanakutana navyo wakiwa porini."Amesema Benoit.

Ameongeza pamoja na kusaidia makundi mbalimbali kuyawawezesha kupata mitungi ya gesi ya Oryx lakini wanajivunia kuwafikia Mama na Baba Lishe zaidi ya 12000 ambao wamepata elimu ya matumizi salama ya kupika kwa gesi sambamba na kuwapatia mitungi midogo na mikubwa kwa lengo la kuwawezesha kufanya shughuli za mapishi kwa urahisi na kuwa salama kiafya,"amesema.

Kwa upande wao baadhi ya Mama na Baba Lishe walioshiriki mashindano ya kupika kwa gesi wamesema kupitia mashindano hayo wamenufaika na mafunzo waliyoyapata sambamba na kuelezwa umuhimu wa kutunza mazingira na wanatoa shukrani kwa waandaaji wakiongozwa na Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Dk.Tulia Ackson.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages