A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, August 27, 2024

MAMA LISHE ,BABA LISHE ZAIDI YA 1000 MKOANI MBEYA WACHUANA MASHINDANO YA KUPIKA KWA GESI YA ORYX

MAMA na BABA LISHE ZAIDI YA 1000 mkoani Mbeya wachuana vikali mashindano ya kupika kwa gesi ya Oryx na Kampuni ya Oryx Gas ikisisitiza lengo la mashindano hayo ni kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia  kama ambavyo Rais Dk.Samia amedhamiria kuhakikisha asilimia 80 ya watanzania iwe inatumia nishati hiyo.
Akizungumza na wana habari mkoani hapa leo Agosti 27,2024 jijini Mbeya , Meneja Miradi ya Nishati Safi kutoka Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Peter Ndomba amesema mashindano hayo yanatija kubwa kwa Mama Lishe na Baba Lishe kwani wanatambua kundi hilo ndilo linaloathirika kiafya kutokana na kutumia kuni na mkaa kwa muda mrefu.

"Mama baba Lishe anakaa muda mrefu anapokua anapopika kwa kutumia  mkaa kwani  tunaambiwa wananchi wengi wa Tanzania wanapoteza maisha kila mwaka kutokana na matatizo ya kupumua au matatizo ambayo yanatokana na madhara ya kuni na mkaa.

"Sasa katika kundi hilo tunaweza kusema Mama na Baba Lishe ndio waathirika wakubwa , hivyo ni jamii ambayo sasa hivi sisi Oryx tunamkakati wa kuhamasisha iachane na matumizi ya Kuni na mkaa. na kuni  na mkaa kwasababu wao ndio wanakaa jikoni muda mrefu katika kupika kila siku ndani ya siku 365,"amesema Ndomba.
Amesisitiza kwa hiyo Mama Lishe na Baba Lishe waanze kubadilika na kuanza kutumia nishati safi hivyo kutawasaidia kukabiliana na changamoto za kiafya na kuokoa maisha yao, mashindano ya kupika kwa gesi ya Oryx kunalenga kuliepusha kundi hilo dhidi ya madhara yanayotokana na matumizi  ya kuni na mkaa.

"Lengo la mashindano haya ni katika muendelezo  ambao Oryx tumeuanza muda mrefu wa kuhamasisha na kusaidia kuhakikisha  matumizi ya nishati safi ya kupikia katika mapishi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages