-Jaji Kiongozi asema NSSF imefungua njia wadau wengine wafuate
Na MWANDISHI WETU, MWANZA
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani amefungua semina kwa njia ya e-Mikutano kwa Waheshimiwa Majaji na Mahakimu wa Kanda ya Ziwa, Tabora, Manyara na Kigoma waliokutana jijini Mwanza. Semina hiyo ni ya siku mbili kuanzia tarehe 9 hadi 10 Juni 2023.
Amesema kupitia semina hiyo NSSF imefungua njia ambayo wadau wengi wataifuata, hivyo Mahakama na NSSF kama ilivyo kwa taasisi nyingine zinazotoa huduma kwa jamii haziwezi kufanikiwa ikiwa kila taasisi itajifungia ikiamini inaweza.
“Niwahakikishie wadau wetu wote wakiwemo NSSF kuwa Mahakama ya Tanzania itaendelea kuwashirikisha katika mipango yake na hususan inapotekeleza mpango mkakati wake wa miaka mitano utakaokamilika ifikapo mwaka 2025,” amesema.
Mhe. Jaji Kiongozi Siyani amesema masuala ya hifadhi ya jamii ni mambo yanayohusu maisha ya watu wakiwa hai au baada ya kuondoka duniani na kuwa malipo ya watu hao hasa yanapohusisha mirathi yamekuwa na changamoto ambapo moja ya mambo yanayoweza kuondoa changamoto hizo ni mawasiliano kati ya Mahakama na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Naye, rais wa Chama Cha Majaji na Mahakimu Tanzania (JMAT), Mhe. Jaji John Kahyoza ameushukuru uongozi wa NSSF kwa kuwawezesha kushiriki semina hiyo ambayo ni moja ya utekelezaji wa malengo makuu ya chama hicho ambacho lengo lake ni kulinda uhuru wa Mahakama na kujenga ujuzi kwa Waheshimiwa Majaji na Mahakimu Tanzania.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani, Godfrey Ngonyani, amesema ushirikiano baina ya Mfuko na mhimili huo ni muhimu na ni sehemu ya mkakati wa NSSF kuendelea kushirikiana na wadau, ikiwemo kuandaa vikao na semina.
Ngonyani amesema Mfuko umekuwa ukishirikiana na Mahakama kupitia ziara ambazo zilifanywa Kanda ya Ziwa, Kanda ya Kaskazini na zinatarajiwa kuendelea katika kanda nyingine na kuwa Mahakama ni wadau muhimu kwenye mashauri dhidi ya waajiri wanaokiuka sheria kwa kushindwa kuwasilisha michango kwa wakati.
Mgeni rasmi Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mheshimiwa Mustapher Mohamed Siyani (akiwa katika picha ya Mkutano mtandaoni) akifungua semina ya siku mbili kwa Waheshimiwa Majaji na Mahakimu wa Kanda ya Ziwa, Tabora,Manyara na Kigoma kwa njia ya mtandao kupitia e-Mikutano kwa lengo la majadiliano kuhusu sheria na majukumu ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF(.
Kauli mbiu ya semina hiyo ni Utoaji wa Haki kwa Wakati kwa Ustawi wa Hifadhi ya Jamii, semina hiyo inafanyika katika ukumbi wa Malaika Jijini Mwanza.
Mhe. Jaji John Kahyoza, rais wa Chama Cha Majaji na Mahakimu Tanzania (JMAT), akizungumza wakati wa Semina ya Waheshimiwa Majaji na Mahakimu wa Kanda ya Ziwa, Tabora, Manyara na Kigoma
Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani, Godfrey Ngonyani, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Masha Mshomba wakati wa Semina ya Waheshimiwa Majaji na Mahakimu wa Kanda ya Ziwa, Tabora, Manyara na Kigoma
Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Mwanza Mhe. Dkt. Ntemi akitoa neno la ukaribisho
wakati wa Semina ya Waheshimiwa Majaji na Mahakimu wa Kanda ya Ziwa, Tabora, Manyara na Kigoma
Meneja wa NSSF Mkoa wa Mwanza Emmanuel Kahensa akiotoa neno la ukaribisho, wakati wa Semina ya Waheshimiwa Majaji na Mahakimu wa Kanda ya Ziwa, Tabora, Manyara na Kigoma Naibu Msajili wa Kanda ya Mwanza, akizungumza wakati wa Semina ya Waheshimiwa Majaji na Mahakimu wa Kanda ya Ziwa, Tabora, Manyara na Kigoma
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Sheria NSSF, Geofrey Sikira akitoa wasilisho kuhusu usimamizi wa Masuala ya Kisheria ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF),wakati wa Semina ya Waheshimiwa Majaji na Mahakimu wa Kanda ya Ziwa, Tabora, Manyara na Kigoma
Mhe. Jaji John Kahyoza, rais wa Chama Cha Majaji na Mahakimu Tanzania (JMAT) (kushoto) akipokea zawadi kwa niaba ya Mgeni rasmi Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mheshimiwa Mustapher Mohamed Siyani kutoka kwa Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani, Godfrey Ngonyani, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Masha Mshomba,wakati wa Semina ya Waheshimiwa Majaji na Mahakimu wa Kanda ya Ziwa, Tabora, Manyara na Kigoma
Mkurugenzi wa uendeshaji, Omary Mziya akitoa neno la utangulizi kuhusu utendaji wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi Jamii (NSSF) na changamoto zake
Meneja Usimamizi wa Mafao James Oigoakitoa mada kuhusu utendaji wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi Jamii (NSSF) na changamoto zake
Meneja Miradi wa NSSF, Helmes Pantaleo akitoa wasilisho kuhusu uwekezaji na Miradi NSSF, kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji na Miradi, Gabriel Silayo
Muwezeshaji wa Semina Austin Makani akiendelea kutoa Muongozo , wakati wa Semina ya Waheshimiwa Majaji na Mahakimu wa Kanda ya Ziwa, Tabora, Manyara na Kigoma Mhe. Jaji Rose Ebrahim, Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Mtwara, akitoa wasilisho kuhusu utekelezaji wa NSSF na changamoto zake.
Majadiliano yanaendelea
Mkutano wa Siku ya kwanza na ya pili ukiendelea
Matukio mbalimbali katika picha
No comments:
Post a Comment