*Filam ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya Royal Tour yaongeza idadi ya watalii
Na Mwandishi Wetu
IDADI ya watalii wanaofika katika hifadhi za Taifa imeongezeka ikilinganishwa na kipindi cha nyuma kutokana na usimamizi bora wa vivutio mbalimbali vilivyopo katika Hifadhi.
Hayo yamesemwa na Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) William Mwakilema ambapo alisema kuwa ongezeko hilo limetokana na filamu ya Royal Tour ambayo ikichangia kuitangaza nchi na vivutio vyake kimataifa.
Filamu hiyo ilifanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ikilenga kutangaza utalii ndani na nje ya nchi, jambo ambalo lilisaidia kuongezeka ka idadi ya watalii.
Mwakilema amesema kuwa Serikali ilifanya maboresho ya miundombinu yake Ili kuhakikisha wageni wanaofika wanatembea Katika mazingira rafiki na salama.
" Filamu ya Royal Tour imesaidia kuongezeka Kwa idadi ya watalii wanaofika kujionea vivutio vya aina mbalimbali, jambo ambalo limesaodia kuongezeka Kwa mapato," amesema.
Amesema kuwa, kwa upande wa hifadhi ya Kilimanjaro idadi ya watalii imeongeza hadi kufikia 259,789 na mapato yaliongezeka hadi kufikia zaidi ya bilioni 78.
"Katika hifadhi ya Serengeti idadi ya watalii imeongezeka na kufika 491,365 na kuingiza mapato zaidi ya sh bilioni 156 ambayo ni nusu ya fedha za mapato ya hifadhi zote huku hifadhi ya Nyerere ikipata watalii 866,632 na kuingiza mapato zaidi ya sh bilioni 89,"amesema.
Mwakilema amesema kutokana na hali hiyo, katika kipindi cha mwaka mmoja wa filamu hiyo, imeingiza jumla ya watalii Serikali imeingiza zaidi ya sh milioni 1,617,796 na mapato ya zaidi ya sh bilioni 324.
Ameongeza kuwa, wakati wanaendelea kupokea watalii, Tanapa iliweza kufanya maboresho ya miundombinu Katika hifadhi mbalimbali ikiwamo Tarangire ,Katavi, Nyerere, Mkomazi, saadani, Serengeti na Mlima Kilimanjaro (KINAPA).
" Tulivyopewa fedha za Covid-19, tulizitumia Kwa kufanya mabiresho ya miundombinu ya kuelekea kwenye hifadhi mbalimbali ikiwamo Kinapa, Tarangire, Hifadhi ya Nyerere, Mkomazi na Sadan, lengo ni kuhakikisha kuwa wageni wakifika wanakaa kwenye mazingira rafiki na salama," amesema na kuongeza kuwa.
" Hifadhi za Mkomazi na Nyerere zimejenga malango ya kuingilia wageni, Nyumba za watumishi na huduma mbalimbali za watalii, wakati katika hifadhi ya Serengeti, Tarangire na Nyerere tumejenga viwanja vya ndege pamoja na hifadhi ya Kilimanjaro (Kinapa) kwa sababu ni mlimani tumejenga viwanja vya uokozi vitano kwenye maeneo ya mkakati ambapo wageni wanapopata changamoto mbalimbali za mlimani tunapelekewa helikopta kwa ajili ya kufanya uokozi,"amesema Mwakilema.
Amesema kuwa, lakini pia katika hifadhi ya Gombe ambayo na yenyewe ipo milimani, wameweza viwanja vya uokozi kwa watalii watakaokuwa wakifika maeneo hayo.
Ameongeza kuwa, lakini pia wameweza kuboresha miundombinu ya barabara kuelekea hifadhini Ili kurahisisha watalii kuwaona wanyama kwa njia rahisi na salama.
"Vifaa mbalimbali vikiwamo magari na vifaa vya ujenzi tumeweza kununua kwa ajili ya kurahisisha shughuli za utalii, jambo ambalo litasaidia kuongeza idadi ya watalii," amesema.
Amesema kuwa, Tanapa imepunguza vitendo vya ujangili na kuimarisha usalama wa wanyama na watalii katika hifadhi za Wanyama.
Kwa upande wake mdau wa sekta ya utalii Mkoani Arusha, Muddy Swali amesema kuwa kite do Cha Serikali kufanya maboresho Katika hifadhi za Taifa kutasaidia kuongeza idadi ya utalii na serikali kupata mapato.
"Watalii wataweza kutumia viwanja vya ndege vilivyopo hifadhini na kufanya shughuli za utalii na kuondoka bila ya usumbufu na serikali itaongeza mapato," amesema Swali.
No comments:
Post a Comment