Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.
Profesa Joyce Ndalichako akiendesha mnada wa kuuza Picha ya kuchora
wakati wakati wa Harambee ya kutegemeza Parokia ya Utatu Mtakatifu
Changanyikeni tarehe 24, Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.
Profesa Joyce Ndalichako akisistiza jambo wakati wa Harambee ya
kutegemeza Parokia ya Utatu Mtakatifu Changanyikeni tarehe 24, Jijini
Dar es Salaam.
Wanaparokia
wa Parokia ya Utatu Mtakatifu Changanyikeni wakifuatilia Harambee ya
kutegemeza Parokia ya hiyo tarehe 24, Jijini Dar es Salaam.
…………………………
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.
Profesa Joyce Ndalichako ametoa wito kwa wanaparokia wa Parokia ya
Utatu Mtakatifu Changanyikeni jijini, kushiriki katika Sensa ya Watu na
Makazi itakayo fanyika tarehe 23 mwezi Agosti 2022.
Akiongea
wakati wa Harambee ya kutegemeza Parokia ya Utatu Mtakatifu
Changanyikeni ambayo imeabatana na kilele cha Sikukuu ya Mavuno leo
tarehe 24, Jijini Dar es Salaam, amesisitiza kuwa zoezi la sensa ni
muhimu kwa Taifa katika kupanga mipango ya maendeleo.
“Serikali
yetu ikiwa na idadi kamili ya watu wa makundi mbalimbali ili kuhakikisha
kuwa rasilimali za nchi zinagawiwa kulingana na mahitaji, hivyo
niwasihi watu wote tujiandae kuhesabiwa”
Aidha, katika hatua
nyingine Mhe. Ndalichako amewapongeza wanaparokia hao hususani
wanajumuiya ambao wamevuka malengo ya kukusanya michango kwa ajili ya
kutegemeza Parokia yao, hivyo amewasihi waendelee kujiwekea hazina kwa
Mwenyezimungu.
“Kila mmoja wetu atoe kwa ajili ya Mwenyezimungu,
ukitoa kwa ajili yake unakuwa umeiweka hazina yako katika mahala
salama, tunapo toa tusiangalie thamani ya kitu bali thamani ya uwekezaji
kwa Mwenyezimungu”
Kwa upande wake Baba Paroko wa Parokia ya
Utatu Mtakatifu Changanyikeni, Padri Gallen Mvungi amewasihi wanaparokia
hao kuendelea kushkamana na kushirikiana katika kutoa michango ili
waweze kufikia malengo ya makusanyo waliyoyaweka kwa mwaka huu.
Shughuli
ya Kutegemeza Parokia hiyo imefanyika siku ya kilele cha Sikuu ya
Mavuno ikiwa na ujumbe kutoka Zab:50-54, Mtolee Mungu Dhabihu za
kushukuru, Mtimizie aliye juu Nadhiri zako.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Monday, July 25, 2022
WAZIRI NDALICHAKO ATIA SHIME USHIRIKI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment