- TESA KIMILIONEA ilikuwa ni wateja na mawakala wa Airtel Money kote nchini.
Dar es Salaam, Jumanne 20 Julai 2022:
Airtel Tanzania leo imekabididhi zawadi kwa washindi wawili wa droo
kubwa ya promosheni ya TESA KIMILIONEA INAEDELEA, mshindi mmoja
amekabidhiwa gari mpya aina ya Toyota RAV4 na wa pili pesa taslimu Tshs
10 milioni.
Washindi
hao ni John Mathayo, mkazi wa Bunju na mfanya biashara wa nyanya na
Ibrahim Dyamwala ambaye ni mkazi wa Goba jijini Dar es Salaam.
Wateja
na Mawakala walikuwa na nafasi ya kuingia kwenye droo ya kwa kutumia
moja ya huduma za kuweka pesa, kutuma pesa Airtel kwenda Airtel, kutoa
pesa, kulipia bili kwa kutumia huduma ya Airtel Money ya promosheni ya
TESA ZAIDI KIMILIONEA na kujishindia Tshs 1 milioni kila siku au gari
mpya aina ya Toyota RAV4 na pesa taslimu Tshs 10 milioni kwenye droo
kubwa.
|
Mkurugenzi
wa Huduma za Airtel Money Isack Nchunda (kushoto) akimkabidhi mfano wa
hundi yenye thamani ya Tshs 10 milioni, Ibrahim Dyamwala ambaye ni
mshindi wa droo kubwa ya TESA KIMILIONEA INAENDELEA jijini Dar es
Salaam. Promosheni ya TESA KIMILIONEA INAENDELEA ilikuwa inawapa fursa
wateja na mawakala wa Airtel Money ya kujishindia Tshs 1 milioni kila
siku au gari mpya aina ya Toyota RAV4 pamoja na pesa taslimu Tshs 10
milioni kwenye droo kubwa ya mwisho kila wana wanavyofanya muamala
wowote kwa kutumia huduma ya Airtel Money. Kulia ni Meneja Uhusiano
Airtel Tanzania Jackson Mmbando na wa pili kushoto ni Meneja Huduma za
Airtel Money Maria Mwamyalla. |
Kwa
upande wake, mshindi wa zawadi ya Tshs 10 milioni Ibrahim Dyamwala
alisema ‘Nilikuwa siamini kama ni kweli Naweza kuwa nimeshinda hii
zawadi ya Tshs 10 milioni. Kwa leo nimeamini na nawashukuru Airtel kwani
kwa sasa nitaweza kukamilisha ujenzi wa nyumba yangu pamoja na kuongeza
uwekezaji kwenye kilimo. Naomba kuwahidi kuwa nitaendelea kutumia
bidhaa za Airtel pamoja na kuwahimiza ndugu, jamaa na marafiki juu ya
umuhimu wa kutumia Airtel Money.
|
Mkurugenzi
wa Airtel Money Isack Nchunda (kulia) akimkabidhi mfano wa ufunguo wa
gari aina ya Toyota RAV4 mshindi wa droo kubwa ya TESA KIMILIONEA
INAENDELEA, John Mathayo ambaye ni mkazi wa Bunju jijini Dar es Salaam.
Promosheni ya TESA KIMILIONEA INAENDELEA ilikuwa inawapa fursa wateja na
mawakala wa Airtel Money ya kujishindia Tshs 1 milioni kila siku au
gari mpya aina ya Toyota RAV4 pamoja na pesa taslimu Tshs 10 milioni
kwenye droo kubwa ya mwisho kila wana wanavyofanya muamala wowote kwa
kutumia huduma ya Airtel Money. |
No comments:
Post a Comment