MBUNGEwa Jimbo la Segerea, wilayani Ilala, mkoani Dares Salaam, Bonnah Kamori, amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki Sensa ya Watu na Makazi, inayotarajiwa kufanyika Agosti 23 mwaka huu ili kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan kuwaletea maendeleo.
Aliyasema hayo, jana, katika matembezi maalumu aliyoyandaa ya kuhamasisha Sensa ya Watu na Makazi pamoja na kumpongeza Rais Samia.
Mbunge Bonnah alieleza, Sensa ya Watu na Makazi ni muhimu kwa maendeleo ya jimbo hilo na taifa kwa ujumla kwani inairahisishia serikalikuandaa mipango yake ya maendeleo.
“Tukihesabiwa itasaidia serikali kupanga bajeti sahihi ya maendeleo kulingana na idadi yawatu. Sensa hii nimuhimu kwa wananchi wa Jimbo la Segerea kwa sababu jimbo hili ndiyo lenye wananchi wengi.
Tanzania nzima, hivyo tukijitokeza kwa wingi ninaamini itasaidia serekali kutuletea maendeleo,”alisema Bonnah.
Alibainisha, sensa itarahisisha serikali kupanga bajeti sahihi kaika kujenga miundombinu bora ya elimu, huduma za afya,barabara, maji na shughuli mbalimbali za maendeleo, hivyo kuwaomba wananchi wa jimbo hilo kujitokeza kwa wingi Agosti 23 kuhesabiwa.
Aliishukuru serikali chini ya Rais Samia kwa kasi kubwa ya maendeleo hapa nchini, kufungua fursa za kiuchumi, kitaifa na kimataifa pamoja na kuwawezesha wananchi kupitia fursa mbalimbali ikiwemo ya mikopo ya asilimia 10 isyo na riba inayotolewa na Halmashauri kwa vikundi vyawajasiriamali wanawake, vijana nawatu wenye ulemavu.
Pia kupitia Filamu ya Tanzania The Royal Tour ambayo alisema imekuwa fursa muhimu ya maendeleo kwa taifa.
Matembezi hayo yalipita katika mitaa mbalimbali ya Kata ya Kiwalani, huku yakihudhuriwa na madiwani wa kata mbalimbali za Halmashauri ya Jiji la Dares Salaam, viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala na wananchi kutoa ndani na nje ya jimbo hilo.
Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Ilala, Said Side, alimpongeza Mbunge Bonnah kwa kuandaa matembezi hayo na kueleza kuwa ufanisi katika Sensa ya Watu na Makazi, utaisaidia serikali chini ya Rais Samia katika utekelezaji wa Ilani ya Chama.
“Wananchi wa Jimbo la Segerea nawaombeni sana. Agosti 23 mwaka huu tujitokeze kuhesabiwa. Ni muhimu kwa maendeleo ya taifa letu. Tunamshukuru Mbunge wetu Bonnah kwa kuliona hili na kuamua kuandaa matembezi haya,”alisema Side.
Diwani wa Viti Maalumu, Betrice Edward, alisema Sensa yaWatu na Makazi ni msingi wa maendeleo kwa taifa lolote katika kuandaa bajeti sahihi hivyo Agisti 23 wananchi wote wanapaswa kushiriki katika sensa.
Aprili 8 mwaka huu, Rais Samia alitangaza rasmi Agosti 23 mwaka huu kuwa Siku ya Sensa yaWatu na Makazi alipokuwa akizindua nembo maalumu ya sensa visiwani Zanzibar.
Tanzania ilifanya Sensa ya Watu na Makazi mara mwaka 2012.
No comments:
Post a Comment