WAZIRI
wa Maji,Nishati na Madini Zanzibar, Mheshimiwa Shahibu Hassan Kaduara
amewataka watumishi wa wizara hiyo kufanya kazi kwa ushirikiano na
juhudi kubwa pamoja na kusimamia nidhamu za watendaji wenzao jambo
ambalo litasaidia kupiga hatua zaidi.
Kauli
hiyo ameitoa jijini Zanzibar wakati alipokuwa kwenye tukio la
makabidhiano ya ofsi baina yake na Waziri aliyekuwepo kwenye Wizara hiyo
baada ya kupangiwa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi na Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi.
Aidha,
Waziri huyo Kaduara amesema kuwa hakuna jambo jema kama ushirikiano na
kama watazungumza lugha moja,nia moja, kazi itakuwa rahisi na badala ya
kutawanyikana lengo la Serikali halitafikia.
"Leo
nimekabidhiwa ofisi mpya ninachowaahidi ni ushirikiano uliotukuka
kikubwa tuendeleze pale tulipoachiwa na Waziri ambaye amemaliza muda
wake na amefanya kazi nzuri ili wananchi wetu waone faida.
"Pia
niwaombe mkasimamie nidhamu ya wataalamu wenzetu tusiende kufukuza
mtu,wala hakuna atakayefukuzwa na hakuna tutakayemuacha bali turekebishe
tabia zetu ili kujenga ufanisi uliotukuka, tukifanya hivyo tutakuwa
wamoja na kufurahia keki hii ambayo tumepewa,"amesema Kaduara.
Nae
Waziri aliyekuwepo awali ambaye amehamishiwa Wizara ya Uchumi wa Buluu
na Uvuvi, Suleiman Masoud Makame amewaomba watumishi kufanya kazi kwa
umoja na kwamba yupo tayari kutoa ushirikiano,ushauri na maoni pale
atakapotakiwa.
"Mimi
nipo tayari kufanya kazi nae lile nililoanza nalo na nilipofikia ili
tuweze kufikia azima ya Serikali , na nimemkabidhi mambo mbalimbali
kuhusu wizara na mashirika yake ikiwemo miradi inayoendelea
mikubwa,"amesema Waziri Suleiman Masoud Makame.Naibu
Waziri wa wizara hiyo, Shabani Ally Othuman amesema kuwa yale yote
yaliyotolewa na Waziri yatatekelezwa kiufanisi ili kazi iweze kusonga
mbele.
No comments:
Post a Comment