KATIKA
Mkutano wa 40 wa CERAWeek unaofanyika jijini Houston nchini Marekani,
Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba ameendelea kuitangaza Tanzania
na hususani mradi wa LNG unaotarajiwa kujengwa mkoani Lindi, Kusini mwa
Tanzania.
Waziri
Makamba alialikwa kama mzungumzaji katika mkutano huo unaojumuisha
zaidi ya nchi 100, washiriki zaidi ya 6,000 na wazungumzaji zaidi ya 840
kutoka serikalini na sekta binafsi wanaoshughulika na sekta ya nishati
duniani.
Waziri
wa Nishati, Mhe. January Makamba akizungumza wakati wa Mkutano wa 40 wa
CERAWeek unaofanyika jijini Houston, Texas. Wengine pichani ni Daniel
Berkove (wa kwanza kushoto), ambaye pia ni mmoja ya waandaji wa Mkutano
wa CERAWeek, Trudi Makhaya (wa pili kutoka kushoto), Mshauri Maalumu wa
Masuala ya Uchumi kwa Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini na Mhe.Dkt.
Mathew Opoku Prempeh, Waziri wa Nishati, Ghana.
Akizungumza
katika mkutano huo, Waziri Makamba amesema, “Tanzania sasa iko tayari
kutekeleza mradi wa LNG na Serikali pamoja na wawekezaji wana nia ya
dhati kabisa kuona mradi huu unakamilika ndani ya muda mfupi ili kuanza
kuvuna kiasi kikubwa cha gesi asilia kilichopo baharini”.
Waziri
Makamba ameeleza kuwa, Tanzania kama ilivyo kwa nchi nyingine za Kusini
mwa Afrika imepiga hatua kubwa katika ukuaji wa uchumi lakini ili
kufikia matamanio ya Serikali na wananchi wake ni lazima kuhakikisha
nchi inakuwa na nishati ya uhakika na ya bei stahamilivu.
Waziri
Makamba aliwaeleza washiriki wa mkutano huo kwamba tayari majadiliano
baina ya Serikali na wawekezaji yanaendelea na lengo ni kufikia
makubaliano ndani ya mwaka 2022.
“Kitu
kingine kizuri kuhusu mradi wa LNG Tanzania ni kwamba gesi yetu ina
kiasi kidogo sana cha hewa ukaa na hivyo kuwa miongoni mwa gesi ambayo
inavutia zaidi wateja duniani kote ukizingatia mikakati ya dunia ya
kupunguza hewa ukaa kwa ajili ya kupunguza athari za mabadiliko ya tabia
nchi,”alieleza zaidi Waziri Makamba.
Mojawapo
ya mada kuu ya mkutano wa 40 wa CERAWeek ni kuhusu mabadiliko ya
matumizi ya nishati kutoka nishati zenye kutoa hewa ukaa nyingi kuelekea
nishati zenye kutoa kiasi kidogo cha hewa ukaa ikiwa ni mikakati ya
kidunia kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.
Waziri
Makamba alieleza baadhi ya mikakati na hatua ambazo Tanzania inachukua
katika kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa ikiwemo kuchochea matumizi ya
gesi asilia katika magari, matumizi ya gesi asilia kuzalisha umeme na
kuondokana na matumizi ya mafuta mazito na pia matumizi ya gesi za
mitungi kwa ajili ya kupikia.
“Asilimia
60 ya umeme katika Gridi ya Taifa inazalishwa na gesi asilia huku
asilimia 40 iliyobaki inatokana na vyanzo vingine ambavyo ni rafiki kwa
mazingira ikiwemo maji,” alisema Waziri Makamba.
Waziri
Makamba aliongeza kuwa, bado kuna changamoto ya kuhakikisha matumizi ya
kuni na mkaa yanapungua na ili kufanikisha hili ni lazima wananchi
wapatiwe vyanzo mbadala vya nishati ambavyo vinaendana na kipato chao na
uhalisia wa maisha yao.
Ujumbe
wa Tanzania uliombatana na Waziri wa Nishati katika Mkutano wa 40 wa
CERAWeek pamoja na wawekezaji katika mradi wa LNG Tanzania ukifuatilia
wasilisho la Waziri Makamba. Kutoka kulia mstari wa mbele ni Naibu
Katibu Mkuu, Ndg. Kheri Mahimbali, Mkurugenzi Mtendaji wa EWURA, Mha.
Godfrey Chibulunje, Kamishna wa Petroli na Gesi kutoka Wizara ya
Nishati, Ndg. Michael Mjinja na Makamu wa Rais na Mwakilishi wa Equinor
Tanzania, Bi. Unni M.S. Fjær. Wengine pichani mstari wa nyuma kuanzia
kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa PURA, Mha. Charles Sangweni, na Makamu
wa Rais na Mwakilishi wa Shell Tanzania, Ndg. Jared Kuehl.
Katika
mkutano huo Waziri Makamba ameambatana na viongozi kutoka Wizara ya
Nishati akiwemo Naibu Katibu Mkuu, Ndg. Kheri Mahimbali, Kamishna wa
Gesi na Mafuta, Ndg. Michael Mjinja, Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt.
James Mataragio, Mkurugenzi Mtendaji wa EWURA,Mhandisi Godfrey
Chibulunje, Mkurugenzi Mtendaji wa PURA, Mhandisi Charles Sangweni
pamoja na maofisa wasaidizi wa viongozi.
No comments:
Post a Comment