JAJI
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Kazi, Mhe. Salma
Maghimbi amewakumbusha watumishi kutumia taaluma zao vizuri na kufanya
kazi kwa uadilifu bila upendeleo.
Sambamba
na kuongeza uwazi na mshikamano mahala pa kazi bila kuathiri maelekezo
ya viongozi ili kusaidia kufanikisha malengo ya Mpango Mkakati wa Awamu
ya Pili.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Kazi, Mhe. Salma
Maghimbi (katikati walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi
wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Kazi wakiwa wamenyoosha mikono
na kutaja neno TEHAMA ikiwa ni salamu ya Devisheni hiyo wakati wa
mafunzo ya siku moja yaliyofanyika leo tarehe 12 Machi, 2022 katika
Ukumbi wa Mikutano wa Mahakama ya Haki Mkazi Kisutu Dar es salaam,
wengine walioketi ni Jaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Mhe.
Augustine Rwizile (wa pili kushoto), Jaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya
Kazi, Mhe. Biswalo Mganga (wa pili kulia), Naibu Msajili, Mhe. Kinabo
Minja (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji na
Tathimini Mahakama ya Tanzania Bw. Sebastian Lacha.
Akizungumza
wakati wa kufungua mafunzo ya Mpango Mkakati wa Mahakama wa awamu ya
pili 2020/2021 hadi 2024/2025 na huduma kwa mteja kwa watumishi wote wa
divisheni hiyo leo tarehe 12 Machi 2022, katika Ukumbi wa Mafunzo Kisutu
jijini Dar es salaam, Mhe. Maghimbi amesema, anatambua kwamba katika
safari ya uboreshaji wa huduma za Mahakama unasimamia nguzo tatu, (3)
ambazo ni Utawala bora na usimamizi wa rasilimali watu, Utoaji haki sawa
na kwa wakati na Ushirikishwaji wa wadau.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Kazi, Mhe. Salma
Maghimbi akitoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya Mpango Mkakati wa
Mahakama wa awamu ya pili 2020/2021 hadi 2024/2025 na huduma kwa mteja
kwa watumishi wote wa divisheni hiyo.
“Naelewa
ilivyo ngumu kujenga jamii yenye uadilifu, kwani misingi ya uadilifu
hujengwa kuanzia kwa wazazi wetu na walezi wetu, lakini kamwe hili
haliwezi kutufanya tukaacha kukumbushana wajibu wetu kama wadau namba
moja wa utoaji haki,” alisema Jaji Mfawidhi
Jaji
Maghimbi ameongeza kuwa, kupitia mafunzo hayo yatawajengea uwezo
watumishi kufahamu mikakati ya Taasisi, kuwaongezea watumishi uadilifu
na pia kuwapa hamasa ya kutoaji huduma za kimahakama zinazoridhisha na
hivyo kuimarisha ushirikiano wa watumishi katika kuboresha huduma.
Aidha,
Jaji Mfawidhi aliwasisitiza washiriki kuwa mada zilizoandaliwa ni
muafaka na zitasaidia kuwajengea uwezo watumishi wa kusimamia na
kutekeleza nguzo ya pili ya Mpango Mkakati wa Mahakama ambao ndiyo
jukumu la msingi lililowekwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ya mwaka 1977 kama ilivyofanyiwa marekebisho mara kadhaa.
Naibu
Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Kazi, Mhe.
Elizabeth Nyembele (wa kwanza kushoto) akiwa miongoni mwa washiliki
akifuatilia mafunzo hayo.
“Inanipa
faraja kubwa kusema uboreshaji wa huduma unaoendelea katika Taasisi
yetu hauna budi kupongezwa na kuungwa mkono na kila mmoja wetu. Ni
dhahiri kwamba kila mmoja analo la kusimulia kwa kuangalia tulipotoka na
mahali tulipo sasa, ni wazi kwamba ilikuwa ni nadra sana kupata fursa
kama hii ya kukutana kwa wingi wetu kama ilivyo sasa na kupata mafunzo”,
alisema Jaji Maghimbi
Jaji
Mfawidhi, alisema kuhusu Taarifa ya REPOA ni tafiti inayotoa tathmini
iliyofanyika kwa Mahakama kupima huduma zinazotolewa ili kujua ni kwa
kiasi gani zina kidhi viwango, hilo litasadia kupima na kurekebisha pale
ambapo hapakwenda sawa kama taratibu za utoaji huduma zinavyopaswa.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Kazi, Mhe. Salma
Maghimbi akimsikiliza mtoa mada wakati wa mafunzo hayo, wengine kwenye
mstari wa mbele ni Jaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Mhe.
Augustine Rwizile (katikati), Jaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi,
Mhe. Biswalo Mganga (wa tatu kutoka kushoto).
“Maoni
yaliyotolewa juu yetu isiwe sehemu ya kuwachukia wateja wetu bali iwe
chachu ya mabadiliko, kibinadamu huwezi kutambua unapokosea isipokuwa
kupitia watu wengine”.aliongeza Jaji Maghimbi
Kwa
upande wa matarajio ya mafunzo hayo Mhe. Maghimbi alisema, ni imani
kubwa baada ya mafunzo hayo watumishi watabadili mienendo yao binafsi na
kushirikiana vizuri na wadau wote, kuwa waaminifu na wakweli katika
utoji wa huduma. Kutotoa huduma kwa upendeleo na kuimarisha ushirikiano
“team work”. Kuongeza uwajibikaji na uwazi kwa kulinda uhuru wa
Mahakama.
Naibu
Msajili, Mhe. Kinabo Minja (aliyesimama mwenye koti jeusi) akitoa mada
ya utafiti uliofanywa na Taasisi ya REPOA kwa Mahakama ya Tanzania
kuhusu viwango vya huduma zitolewazo na Mahakama kwa mteja
Jaji
Maghimbi alihitimisha kwa kuwashukuru Shirika la Kazi Duniani (ILO) kwa
mchango wake mkubwa wa kufanikisha mafunzo hayo “Nitakuwa mchoyo wa
fadhila endapo sitatoa shukrani za dhati kwa wawezeshaji wa mafunzo haya
Shirika la Kazi duniani na wale wote ambao wameshiriki katika
maandalizi ya mafunzo haya,"amesema.
Sehemu ya watumishi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Kazi, waliohudhuria mafunzo hayo wakifuatilia mafunzo hayo.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Mahakama ya Tanzania Bw.
Sebastian Lacha (aliyesimama mbele) akitoa mada ya Mpango Mkakati wa
Mahakama wa awamu ya pili wa mwaka 2020/2021 hadi 2024/2025 wakati wa
mafunzo hayo.
Sehemu
ya watumishi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Kazi,
waliohudhuria mafunzo hayo wakifuatilia mafunzo hayo.(Picha na Innocent
Kansha - Mahakama)
No comments:
Post a Comment