TIMU ya taifa ya wasichana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17 (U17) imefanikiwa kwenda Raundi ya Tatu kufuzu Kombe la Dunia.
Ni
baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya wenyeji, Botswana kupitia
mtanange wa Machi 20,2022 uliopigwa katika dimba la Obeid Itan Chilume
lililopo Francistown, Botswana.
Neema Kinega dakika ya 28 alianza kuwapa raha Watanzania na baadaye Clara Luvanga akatupia mabao matatu dakika za 62, 63 na 81.
Kutokana
na matokeo hayo, Tanzania inafuzu kwa ushindi wa jumla ya mabao 11-0
kufuatia kuwachapa Botswana 8-0 kwenye mechi ya kwanza jijini Zanzibar.
Aidha,
mtanage ujao unatarajiwa kupigwa kati ya Tanzania na Burundi kutafuta
nafasi ya kuingia hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania tiketi ya India
baadaye mwaka huu.
Watanzania wameonesha kuwa na furaha baada ya timu hiyo ya wasichana kuwapa heshima ya kipekee katika michuano ya Kimataifa
No comments:
Post a Comment