Na Mwandshi Wetu
Wafanyabiashara
Jijini Dodoma waikubali huduma ya LIPA KWA SIMU inayotolewa na Mtandao
nambari Moja unaoongoza kwa mapinduzi ya Kidigitali Tigo Tanzania,
ambapo sasa Tigo inatoa ofa na Promosheni mbalimbali za kusisimua kwa
wateja wake hasa kuelekea Serengeti Music Festival 2022.
Akithibitisha
hilo , Meneja wa Huduma za Malipo Tigo - Pesa Bwana Reuben Kamuga
amesema kuwa Tigo wanatambua umuhimu wa kuenzi tamaduni za kitanzania,
kukuza tasnia za muziki nchini, kukuza vipaji vya wasanii wachanga ,
kuibua fursa za kibiashara , na kutoa elimu ya ujasiriamali katika
maeneo mbalimbali nchini .
"Kuendana na shangwe la Serengeti
Music Festival 2022 kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya Kidigitali hapa
nchini Tigo inatoa huduma, Ofa na Promosheni mbalimbali za kusisimua.
Kupitia huduma ya LIPA KWA SIMU kwa kushirikiana na bar mbalimbali hapa Dodoma.
Dunia Sasa hivi Ipo kiganjani kupitia simu ya mkononi sasa unafanya
Malipo popote ukiwa na huduma ya LIPA KWA SIMU ambapo kwenye tamasha
hili la Serengeti Music Festival 2022 wateja wa Tigo wataweza kulipia
vinywaji na vyakula Kidigitali huku wakiendelea kupata burudani.
Tunawakaribisha
wateja wetu kufurahia Ofa hizi kutoka Tigo lakini pia kujumuika nasi
katika viwanja vya Chinangali weekend hii ili tuweze kujumuika pamoja"
alisema bwana Kamuga
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Chanangali
Park Bwana Frank Ngonyani amewakaribisha wakazi wa Dodoma kutembelea
viwanja ivyo kwa ajili ya Kushuhudia Serengeti Music Festival 2022
ambapo mdau mkubwa katika Tamasha Hilo ni Tigo Pesa , Aidha amewapongeza
kwa kuendelea kuwa wabunifu na kutoa huduma za Kidigitali kwa wateja
wake.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Saturday, March 12, 2022
Home
BIASHARA.
WAFANYABIASHARA DODOMA WAIKUBALI HUDUMA YA LIPA KWA SIMU KUELEKEA SERENGETI MUSIC FESTIVAL 2022
WAFANYABIASHARA DODOMA WAIKUBALI HUDUMA YA LIPA KWA SIMU KUELEKEA SERENGETI MUSIC FESTIVAL 2022
Tags
BIASHARA.#
Share This
About kilole mzee
BIASHARA.
Labels:
BIASHARA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment