Baadhi
ya wageni walioendelea kutembelea Banda la NEMC wakiendelea kupata
elimu jinsi usimamizi na utunzaji wa Mazingira nchini Tanzania
unavyofanyika kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu.Miongoni
mwa wageni waliotembea banda la NEMC nchini Qatar ni mke wa Balozi wa
Tanzania (katikati aliyevaa mtandio kichwani), Bi. Safia Mahadhi ambaye
ameipongeza NEMC kwa kushiriki maonesho hayo na kuwashauri kuwa yale
mazuri waliyojifunza wayapeleke nchini Tanzania kwa lengo la kuboresha
mazingira na fursa za uwekezaji nchini.Leo
tarehe tarehe 13/3/2022 Banda la NEMC nchini Qatar lilitembelewa na
balozi wa Tanzania ( katikati) Mh. Dkt. Mahadh Maalim pamoja na balozi
wa Kenya (wa pili kulia) nchini Qatar Mh. Paddy Ahenda wamepongeza NEMC
kwa kushiriki maonesho makubwa ya Kimataifa ya Kilimo na Mazingira na
kuwashauri waendeee kutumia fursa kama hizi ili kutoa elimu na
kuitangaza nchi kupitia hifadhi na utunzaji wa Mazingira. Bodi
ya Kahawa yaendelea kuvutia wanunuzi wa Kahawa nchini Tanzania kupitia
maonesho ya Kimataifa ya Kilimo na Mazingira nchini Qatar.Wizara ya Mambo ya Nje yaendelea kung'ara maonesho ya Kimataifa ya Kilimo na Mazingira nchini Qatar.
Mteja akisikilizwa kwenye Banda la NEMC nchini Qatar Baraza
la Taifa la Hifadhi na Usimamzi wa Mazingira (NEMC) wametembelea
Kampuni ya Elite Paper Recruiting nchini Qatar inayojishughulisha na
urejerezaji wa taka za karatasi. Kampuni hii inakusanya taka za karatasi
toka maeneo mbalimbali nchini Qatar na kuzirejereza ili kupata bidhaa
za karatasi. Hivyo, Kampuni hii inasaidia kupunguza ukataji wa miti kwa
ajili ya kutengeneza bidhaa za karatasi hivyo inasaidia kutunza
Mazingira hususani katika kukabiliana na changamoto za Mabadiliko ya
Tabianchi. Kampuni hii inasambaza bidhaa zake katika mataifa mbalimbali
ikiwemo Tanzania hivyo ni fursa nzuri kwa Tanzania kupitia NEMC
kushirikiana nao kuanzisha viwanda vya kurejereza taka za karatasi kwa
lengo la kupunguza uchafuzi wa Mazingira na kuongeza fursa za ajira
nchini.
No comments:
Post a Comment