SERIKALI
imesema inaendelea kuweka mikakati madhubuti juu ya namna ya kujikinga
na kukabiliana na maafa ili kuepuka madhara makubwa yanayoweza
kujitokeza na kuhatarisha usalama wa raia pamoja na kuharibu
miundombinu.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. Balozi.
Dkt.Pindi Chana akizungumza wakati wa semina kwa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu dhana na Mfumo wa Usimamizi wa Maafa
nchini iliyofanyika Machi 12, 2022 katika Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.
(Picha zote na OWM).
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na
Uratibu, Mhe. Balozi Dkt.Pindi Chana katika semina kwa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu dhana na Mfumo wa Usimamizi wa
Maafa nchini iliyoandaliwa na Idara ya Menejimenti ya Maafa katika
Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.
Baadhi
ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakichangia
hoja katika semina hiyo kuhusu dhana na Mfumo wa Usimamizi wa Maafa
nchini iliyofanyika Machi 12, 2022 katika Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Dkt.Joseph Mhagama
akieleza jambo wakati wa semina kwa kamati hiyo kuhusu dhana na Mfumo wa
Usimamizi wa Maafa nchini iliyofanyika Machi 12, 2022 katika Ukumbi wa
Bunge jijini Dodoma.
“Hivi
sasa Mheshimiwa Mwenyekiti nikuhakikishie elimu inayotolewa katika
shule zetu za Msingi Sekondari na ngazi ya vyuo vikuu inalenga vijana
wetu na jamii yetu kujua maafa kwa ujumla ili kujikinga wasipate
madhara,”amesema Mhe.Pindi.
Aidha,
alibainisha kwamba utafiti unaofanywa na watalaamu mbalimbali kuhusu
Mazingira na Maafa utumike vyema kama moja ya njia ya kukabili maafa ya
asili na yale yatokanayo na shughuli za kibinadamu. Utafiti hutoa mwanya
wa kujua hatua sahihi za kuchukua kabla ya majanga kutokea na baada ya
kutokea.
Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Bw. Kaspar
Mmuya akifafanua jambo wakati wa semina kwa Kamati hiyo kuhusu dhana na
Mfumo wa Usimamizi wa Maafa nchini iliyofanyika Machi 12, 2022 katika
Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.
Wakati
huo huo Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu,
Bw. Kaspar Mmuya alifafanua kwamba Muswada wa Sheria ya Maafa utasaidia
kuondoa changamoto zilizobainika kutokana na sheria ya zamani na
wahusika kufahamu majukumu yao ili kuepusha muingiliano wa majukumu
wakati wa utekelezaji wa shughuli zote za maafa.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. Balozi
Dkt.Pindi Chana akizungumza wakati wa semina kwa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu dhana na Mfumo wa Usimamizi wa Maafa
nchini iliyofanyika Machi 12, 2022 katika Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.
Naye
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria,
Mhe. Najma Giga alishauri Mfuko wa Maafa kutengewa bajeti yake
itakayosaidia kutatua changamoto zinazotokana na Maafa badala ya
kusubiri hadi yatokee na kuanza kutafuta wadau kwa ajili ya kutoa
huduma.
“Tunaelewa
waziwazi kuna Maafa ya kimaumbile ambayo huwenda yakatokea kila mwaka
kutokana na mvua za masika au mabadiliko ya tabianchi kwenye fukwe zetu
za bahari tunajua kabisa kila mwaka mabadiliko ya tabia nchi
yanapotokea shemu ya ardhi inaliwa lakini ikitokea Maafa ndio tunaanza
kupambana kutafuta wadau. Mfuko unaanza kutuna kwanini sasa serikali
isione utaratibu utakaowekwa maalumu kwa hao hao watu
wanaotusaidia,”alieleza Makamu Mwenyekiti huyo.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,
Bunge na Uratibu,Bw.Charles Msangi akiwasilisha Dhana na Mfumo wa
Usimamizi wa Maafa Nchini katika semina kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Katiba na Sheria iliyofanyika Machi 12, 2022 katika Ukumbi wa Bunge
jijini Dodoma.
Akihitimisha
wasilisho la dhana na Mfumo wa Usimamizi wa Maafa katika semina hiyo
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Bw. Charles Msangi alisema Muswada wa
Sheria imezingatia uwajibikaji wa wadau wote kwani ulifanyika utafiti
ambao uliangalia majukumu ya kila muda.
No comments:
Post a Comment