WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na
Watu Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako amesema Serikali ya Awamu ya
Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria
kutoa fursa kwa vijana nchini ili waweze kuondokana na changamoto ya
ajira.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.
Prof. Joyce Ndalichako akizungumza jambo na kijana mwenye ulemavu Bw.
Marko Palanjo mnufaika wa mafunzo hayo ya kilimo cha kisasa kwa utumia
teknolojia ya kitalu nyumba yanayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
(Picha zote na OWM-Kazi, Vijana, ajira na Wenye Ulemavu).
Waziri
Ndalichako ameyasema hayo Machi 19, 2022 alipoambatana na Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walipotembelea mradi wa Kitalu
Nyumba (Greenhouse) katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa lengo la
kukagua maendeleo ya mafunzo hayo ya kilimo cha kisasa yanayoratibiwa na
Ofisi ya Waziri Mkuu.
Amesema
kuwa, katika kufanikisha hilo Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu
imekuwa ikiratibu Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi ambayo imelenga
kuwezesha nguvu kazi ya Taifa kupata ujuzi na stadi za kazi stahiki ili
kumudu ushindani wa soko la ajira na kuwawezesha kujiajiri au kuajiri
wenzao.
“Mheshimiwa
Rais amedhamiria kutoa fursa zaidi kwa vijana nchini na serikali
anayoiongoza imekuwa ikiwapatia vijana fursa mbalimbali ikiwemo ujuzi na
stadi za kazi ili waweze kushiriki kwa ufanisi katika shughuli za
uzalishaji mali sambamba na kuongeza fursa za ajira,” alisema Waziri
Ndalichako.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana,
Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (kulia) akieleza
jambo alipofanya ziara na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba
na Sheria kwa lengo la kukagua mradi huo Wilaya ya Meru, Mkoani Arusha.
Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe.
Asha Abdalla.
Sehemu
ya vijana wakisikiliza maelezo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (hayupo
pichani) walipotembelea mradi wa kitalu nyumba kwa lengo la kukagua
maendeleo ya mafunzo waliyopatiwa kupitia teknolojia ya kilimo cha
kisasa cha Kitalu Nyumba (Greenhouse) Machi 19, 2022 Meru, Mkoani
Arusha.
Aliongeza
kuwa, Serikali imetenga shilingi bilioni 9 kwa ajili ya kutekeleza
Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi kupitia mafunzo ya uanagenzi, mafunzo
ya utarajali (Internship Training), mafunzo ya kurasimisha ujuzi
uliopatikana katika mfumo usio rasmi wa mafunzo na mafunzo ya kilimo cha
kisasa kwa kutumia kitalu nyumba (Greenhouse Farming Training).
Akizungumzia
mafunzo hayo ya Kilimo cha Kisasa kwa kutumia teknolojia ya Kitalu
Nyumba, alisema kuwa zaidi ya vijana 702 kutoka katika halmashauri 7
mkoani Arusha wamenufaika na mafunzo hayo ambapo vijana hao wamepatiwa
mafunzo ya nadharia na vitendo ya ujenzi wa kitalu nyumba pamoja na
kilimo ndani ya kitalu nyumba (Greenhouse).
Aidha,
Waziri Ndalichako alitoa wito kwa Viongozi wa Halmashauri kuhakikisha
wanatekeleza maagizo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Kassim Majaliwa kwa kuwezesha vijana vitendea kazi kupitia
mikopo ya asilimia 10 inayotokana na mapato ya ndani (4% Vijana, 4%
Wanawake na 2% Watu wenye Ulemavu) ili kuwawezesha vijana hao kufanya
kazi au shughuli zenye tija.
Sambamba
na hayo, amewataka vijana kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotolewa na
serikali yao ili waweze kunufaika pamoja na kushiriki katika kusukuma
gurudumu la maendeleo.
Kiongozi
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mhe. Adam Mwakasaka
(wa kwanza kulia) akieleza jambo wakati wa ziara hiyo. Wa pili kutoka
kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako.
Katibu
Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu)
Prof. Jamal Katundu akifafanua jambo wakati wa ziara hiyo ya Wajumbe wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walipotembelea mradi wa
kitalu nyumba Wilaya ya Meru, Mkoani Arusha.
Kwa
upande wake, Kiongozi wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria,
Mhe. Adam Mwakasaka alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita kwa
kushirikiana na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa
ikipitisha bajeti kwa ajili ya kuwezesha utekelezaji wa programu hiyo
ili kuwezesha nguvu kazi ujuzi unaotakiwa katika soko la ajira.
Naye
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye
Ulemavu) Prof. Jamal Katundu alisema kuwa ujuzi huo waliopatiwa vijana
kwa ufadhili wa serikali yao umekuwa ni chachu ya kuwawezesha wajiajiri
katika sekta ya kilimo.
Hali
Kadhalika alielezea mipango ya ofisi hiyo namna ilivyojipanga kuongeza
wigo wa mafunzo hayo ili kuwafikia vijana katika maeneo mbalimbali ya
nchini.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.
Prof. Joyce Ndalichako akiwa ameambatana na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Katiba na Sheria walipotembelea mradi wa kitalu nyumba
Wilaya ya Meru, Mkoani Arusha.
Mnufaika
wa Mafunzo Bw. Pendael Mollel (kushoto) akieleza jambo kwa Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.
Prof. Joyce Ndalichako (wa pili kutoka kulia) pamoja na Wajumbe wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walipotembelea mradi wa
kitalu nyumba Wilaya ya Meru, Mkoani Arusha. Wa pili kutoka kushoto ni
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Zainab Makwinya.
Akitoa
neno la shukrani mnufaika wa mafunzo hayo, Bi. Mariam Juma alishukuru
serikali kwa kuwapatia mafunzo hayo ambayo yamewapa hamasa vijana wengi
wa mkoa huo kutambua manufaa yaliyopo kwenye kilimo hicho, waliahidi
kuendeleza ujuzi huo kwa wananchi ili uwasaidie kuwakomboa kiuchumi.
“Tunamshukuru
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutambua mchango wetu sisi
vijana hakika hatuta muangusha, tutatumia ujuzi tuliopata kujikomboa
kiuchumi,” alisema.
No comments:
Post a Comment