Naibu
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi-Uchukuzi, Atupele Mwakibete akitoa
maelekezo kwa Meneja wa Bandari ya Ziwa Viktoria, wakati alipotembelea
Bandari ya Kemondo, Mkoani Kagera.
Naibu
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi-Uchukuzi, Atupele Mwakibete (katikati),
pamoja na Viongozi mwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)
wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa mzani uliojengwa katika bandari ya
Kemondo, Mkoani Kagera.
Gari la mizigo likipima katika mzani mpya uliojengwa katika Bandari ya Kemondo Mkoani Kagera.
Naibu
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,-Uchukuzi Atupele Mwakibete akimsikiliza
Karani kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Dalila
Shakiru, Wakati akimweleza namna hatua za upimaji zinavyofanyika, mara
baada ya Naibu Waziri huyo kuzindua rasmi matumizi ya mzani huo katika
bandari ya Kemondo, Mkoani Kagera.
Kaimu
Meneja wa Bandari za Ziwa Viktoria, Vicent Stephen akifafanua kwa Naibu
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi-Uchukuzi, Atupele Mwakibete kuhusu
maboresho ya bandari ya Bukoba, wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea
Bandari hiyo Mkoani Kagera.
Naibu
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete akitoa maelekezo kwa
Kaimu Meneja wa Bandari ya Ziwa Viktoria, Vicent Stephen (wa tatu kulia)
wakati alipotembelea Bandari ya Bukoba, Mkoani Kagera.
PICHA NA WUU
……………………………………………….
Naibu
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete, amesema kuwa
kukamilika kwa ujenzi wa mzani katika bandari ya Kemondo mkoani Kagera
ni miongoni mwa mwendelezo wa njia zinazotumika kupata idadi halisi ya
mzigo unaoingia na kutoka bandarini hapo ili kudhibiti mianya ya upotevu
wa mapato.
Amezungumza hayo mkoani Kagera, wakati akifungua
rasmi mzani huo ambao umekamilika kujengwa kugharimu kiasi cha shilingi
milioni 34.
Naibu Waziri huyo amesema Serikali ya Awamu ya Sita
imejikita katika kukusanya mapato hivyo itaendelea kuwekeza fedha
kwenye miudombinu ili kuziimarisha kimapato na kuongeza tija.
“Kumekuwa
na mianya mingi ya upotevu wa mapato katika maeneo mbalimbali hivyo
tunaimarisha miuondombinu sambamba na mifumo hivyo nina Imani uwepo wa
mzani huu tutajua sasa mzigo unaoingia na kutoka na kudhibiti mapato”,
amesema Naibu Waziri Mwakibete.
Naibu Waziri Mwakibete ameitaka
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), kuharakisha taratibu za
manunuzi kwa ajili ya mradi upanuzi wa bandari ya Bukoba, Kemondo na
Mwanza ili kwenda sambamba na ukamilikaji wa meli ya MV Mwanza.
Aidha,
Naibu Waziri Mwakibete ameongeza kuwa pamoja na utekelezaji wa miradi
hiyo Mamlaka ihakikishe miradi yote inazingatia thamani ya fedha ili
kukamilika kwa ubora.
Naye Kaimu Menenja wa Bandari za Ziwa
Viktoria, Vicent Stephen, amesema maboresho yaliyofanywa kwa bandari ya
Kemondo yameongeza huduma ya shehena kufikia tani 9,652 kwa mwaka 2022
ikilinganisha na tani 3,436 kwa mwaka 2021 na kupandisha mapato kufikia
milioni 165 kwa mwaka 2022 kulinganisha na 108 kwa mwaka 2021.
Stephen
ameongeza kuwa kwa mwaka 2021/22 Mamlaka imetenga bilioni 8 kwa ajili
ya kuboresha gati, jengo la abiria, uzio na miuondombinu mingine katika
bandari ya Kemondo ili kuruhusu meli ya MV Mwanza kapakia na kupakua
mizigo itakapoanza huduma.
Naibu Waziri wa Ujenzi na
Uchukuzi-Uchukuzi, Atupele Mwakibete yuko mkoani Kagera kwa ziara ya
siku mbili kukagua maendeleo ya miradi mbalimbali ya sekta inayoendelea
mkoani humo.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Monday, March 21, 2022
NAIBU WAZIRI MWAKIBETE AFUNGUA MZANI KATIKA BANDARI YA KEMONDO
Tags
LOCAL#
Share This
About kilole mzee
LOCAL
Labels:
LOCAL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment