Balozi wa Korea nchini Kim Sun
Pyo amezindua rasmi Chumba Cha Kutakasia Vifaa Tiba kilichopo katika
Hospital ya Rufaa ya Tumbi iliyopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.
Akizungumza
mara baada ya uzinduzi huo Balozi Pyo alisema kuwa uzinduzi huo
umefanyika mara baada ya kumalizika kwa ukarabati wa majengo hayo
uliotokana na ufadhili wa Taasisi ya Kikorea inayofahamika kwa jina la
Korea Foundation for International Healthcare (KOFIH).
Kwa upande
wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Tumbi Amani Malima
alisema kuwa Hospital hiyo imeongeza wigo wa utoaji wa huduma za Afya
ambapo hivi sasa inahudumia wagonjwa wengi zaidi wanaofika Hospitalini
hapo baada ya kupata Rufaa ,wasio na wenye Rufaa kutoka ndani na nje
ya Mkoa wa Pwani.
Mganga Mfawidhi Malima aliongeza kwa kusema
kuwa Hospital hiyo wanapokea majeruhi wengi wa ajali kwa kuwa wako
pembezoni mwa barabara kubwa iendayo Mikoani.
"Kutokana na
ongezeko la uhitaji wa vifaa tiba safi na salama vilivyotakaswa kwa
kufuata sheria na taratibu za kitabibu , ili kukidhi mahitaji ya
wagonjwa ambao ni majeruhi wahitaji wa huduma za upasuaji huduma za
kusafisha vidonda na huduma nyingine zinazohusiana na hizo, Uongozi wa
Hospitali ulifikia hatua ya kuona umuhimu wa kuwa na Chumba Cha
Kutakasia Vifaa ambacho kitarahisisha upatikanaji wa huduma za utakasaji
wa vifaa kwa wagonjwa ili kupunguza maambukizi"alisema
Malima
alisema kuwa mradi mzima wa kukarabati Chumba Cha Kutakasia Vifaa
umegharimu kiasi cha Mil 232,560,000 huku vifaa na ukarabati wa vyumba
vya Kutakasia ukigharimu kiasi cha Mil.52,630,000 na ununuzi wa mashine
pamoja na kusimika ni Mi.179,930,000.
Wakati
huohuo Mganga Mkuu w Mkoa wa Pwani Dkt. Gunini Kamba alisema
wamemtembeza Balozi Pyo kwenye jengo la watoto njiti ambapo kwa siku
hupokea watoto kati ya 30 hadi 40 ambao wanazaliwa kabla ya umri wa
miezi sahihi ya kuzaliwa.
"Hapo awali hatukuwa na majengo haya
ambapo baada ya ukarabati mkubwa uliofanyika sasa hali ya kutunza
watoto hawa ambao almaarufu kama njiti umekuwa rahisi na salama kwa
mama na mtoto"alisema Dkt. Gunini.
No comments:
Post a Comment