A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, March 12, 2022

MRADI UPANUZI WA BANDARI YA TANGA KULETA MANUFAA MAKUBWA

 Mradi mkubwa wa upanuzi wa bandari ya Tanga umefikia asilimia 26 wa ujenzi wake huku ukitarajiwa kukamilika Oktoba mwaka huu

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika maonesho ya TANZFOOD,Mhandisi Hamis kipalo alisema mradi huo upo nyuma ya muda kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo ya ugonjwa wa Covid 19 iliyosababisha nchi nyingi kufunga mipaka

"Ugonjwa wa Covid 19 ulisababisha vifaa vya ujenzi kutoingia nchini kutokana na nchi nyingi kufunga mipaka yao"alisema Mhandisi Kipalo

Aliongeza kuwa mradi huo ukikamilika utaleta manufaa makubwa kwa nchi katika kuongeza ufanisi wa bandari kutoka tani laki saba na nusu hadi tani Milioni 30

"Uwezo wa bandari utaongezeka na pia itasaidia biashara katika ukanda wa kaskazini na Afrika Mashariki "alisema Mhandisi Kipalo

Naye Afisa uhusiano wa bandari ya Tanga,Adam Shindo alisema ushiriki wao katika maonyesho hayo ni kusogea karibu na wateja wao nakutumia fursa hiyo kwa kujitangaza zaidi

"Kilichotuleta hapa ni kusogea karibu na wateja wetu na kuwaelezea maendeleo ya mradi,upanuzi wa bandari ya tanga "alisema Shindo

Mradi huo unatekelezwa na kampuni ya CHEC kutoka China na kusimamiwa na Mhandisi mshauri kutoka Denmark ikishirikiana na kampuni ya Kitanzania Anova

Afisa uhusiano wa bandari ya Tanga Adam Shindo akizungumza na vyombo vya habari katika maonyesho ya kimataifa TANZFOOD jijini Arusha

Mhandisi Hamisi Kipalo akizungumza na waandishi kuhusu maendeleo ya mradi mkubwa wa upanuzi wa bandari ya Tanga

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages