A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, March 3, 2022

KWARESMA NI KIPINDI CHA KUJINASUA

Adeladius Makwega-DODOMA Wakristu wametakiwa kutumia wakati wa Kwaresima kuacha mambo mabaya na kumrudia Mungu kwani kwa kufanya hivyo kwa hakika wengi wanaweza kuwa wema na kuachana na mambo mabaya mara baada ya kwisha mfungo huo wa siku 40 na dunia kuwa sehemu salama. 

 Kauli hii imetolewa siku ya Jumatano ya Majivu ya Machi 2, 2022 katika misa ya majivu katika Kanisa Katoliki la Bikira Maria Imakulata Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma na Paroko wa Parokia hiyo Padri Paul Mapalala. “Kila mkristu aingie ndani ya nafasi yake ajiulize na kujitafiti na ajikabidhi kabisa kwa Mungu wakati tunasubiri sikukuu ya pasaka.”

 Aliendelea kwa kusema kuwa Kipindi cha Kwaresma ni wakati wa kujipatanisha baina ya mtu na Mungu na mtu na mtu akiongeza kuwa muda huu ni wa sala, kufunga na kuwasaidia masikini. Kiongozi huyu wa kanisa katoliki alisisitiza juu ya kuachwa kwa tabia ya utoaji wa mimba kwani hilo ni si jambo jema.

 Katika misa hiyo waamini hao walipata nafasi ya kupakwa majivu ambayo ilielezwa kuwa ni ishara ya kukumbuka kuwa binadamuani mavumbi na mavimbini atarudi.

Pia akisema kuwa hii ni ishara ya kuwa binadamu si mkamilifu. Kipindi hicho cha Kwaresma kitadumu kwa siku 40 ambapo kitahitishwa na Jumapili ya Pasaka ambayo ndiyo Pasaka yenyewe.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages