KAMATI
ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji imeitaka Serikali kuwekeza
nguvu zaidi katika kutoa elimu kwa umma juu ya udhibiti wa sumukuvu ili
kupunguza madhara yanayosababishwa na sumukuvu.
Hayo
yamesemwa leo wilayani Kibaha,Mkoa wa Pwani na Mwenyekiti wa Kamati ya
Bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji,Dkt. Christine Ishengoma katika ziara ya
ukaguzi wa ujenzi wa karantini na maabara ya Kituo cha Udhibiti wa
Magonjwa ya Kibailojia ya Mimea (National Biocontrol Unit) chini ya
mradi wa UDHIBITI WA SUMUKUVU.
“Tunaipongeza
Serikali kwa ujenzi wa maabara ya udhibiti wa magonjwa ya kibaolojia ya
mimea,ambayo kukamilika kwake kutasaidia sana kupunguza matumizi ya
kemikali kama viuatilifu katika mimea katika kudhibiti magonjwa na
mashambulio ya wadudu waharibifu katika mimea.
"Mkandarasi
wa majengo haya lazima ahakikishe kwamba majengo haya yanakamilika kwa
wakati na kwa ubora wa vigezo vya kimataifa vya maabara ya aina hii.
"Aidha
serikali ihakikishe inatoa elimu kwa umma na hasa kwa wakulima wadogo
wadogo juu ya udhibiti wa sumukuvu katika mimea na kuelimisha wakulima
juu ya matumizi ya wadudu marafiki katika kudhibiti magonjwa ya
mimea,”amesema Dkt.Ishengoma.
Akitoa
maelezo ya awali Naibu Waziri wa Kilimo,Mhe. Anthony Mavunde
ameishukuru Kamati ya Bunge kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kusimamia na
kuishauri serikali katika masuala yahusuyo kilimo na kuahidi kuyafanyika
kazi maelekezo yaliyotolewa.
Mhe.Mavunde
aliongeza kwamba katika utekelezaji wa mradi huo wa UDHIBITI WA
SUMUKUVU,serikali imeweka lengo la kuwafikia na kutoa elimu kwa wakulima
60,000,Maafisa Ugani 1351,Wafanyabiashara 5000 na Waandishi wa Habari
100 pamoja na kuwajengea uwezo wataalamu kwa kufadhili shahada za
Uzamivu (PhD) kwa wataalamu watano na Shahada za Uzamili 19.
Katika
mradi huu wa UDHIBITI WA SUMUKUVU pamoja na ujenzi wa maabara ya
utafiti kwenye Kituo cha Taifa cha Udhibiti Magonjwa ya Mimea Kibaha pia
utahusisha utekelezaji wa miradi mingine katika mikoa 10 ya Tanzania
Bara na Zanzibar itakayohusisha;
>Kujenga maghala 14 ya kuhifadhi mazao ya chakula;
>Ujenzi wa kituo mahiri cha usimamizi wa mazao baada ya kuvuna (Post harvest Center of Excellency)
>Ujenzi wa Maabara Kuu ya Kilimo.
No comments:
Post a Comment