Kaimu
Katibu wa Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC) Tawi la Arusha Asha Rashid
akimkabidhi Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Arusha girls box la taulo
za kike mara baada ya kumaliza Kampeni ya uongozi wa Shirika hilo
kutembelea baadhi ya shule za Sekondari nchini kugawa taulo kama sehemu
ya Kuadhimisha Siku ya Wanawake Dunia.
Picha
ya pamoja ya uongozi wa Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC) wakiwa na
Katibu wa Shirika hilo Asha Rashid wakiwa katika shule ya Sekondari
Arusha girls mara baada ya kukabidhi taulo za kike wakisikiliza machache
kutoka Kwa wenyeji wao.
KAMPENI
ya ugawaji wa taulo za kike Kwa baadhi ya shule iliyoandaliwa na
Shirika la Bima Zanzibar (ZIC) lahitimishwa rasmi katika wiki ya
Kuadhimisha Siku ya Wanawake Dunia Mkoani Arusha.
Akizungumza
na wanafunzi pamoja na walimu ,Kaimu Katibu Mkuu wa Shirika la Bima la
Zanzibar (ZIC) Mkoa wa Arusha ,Asha Rashid mara baada ya kutembelea
shule ya Sekondari Arusha girls amesema ni muhimu jamii inayomzunguka
mtoto wakike iwe chachu na silaha ya kumjengea uwezo na Mazingira rafiki
Binti na kujiona wa fahari pale anapokuwa kwenye Hedhi Ili aweze
kujiamini.
"Hedhi
sio ugonjwa Wala sio kitendo Cha aibu hivyo ni muhimu jamii ikatambua
kuwa wanayohaki ya kuhakikisha binti huyo anajikubali na kuendelea na
Majukumu yake ya kimasomo Huku ikimuhakikishia anapata taulo Kwa mlengo
wa kujihifadhi kabidhi taulo za Kike awapo shuleni."
Aidha,kaimu
huyo ameeleza lengo la kuchagua shule ya Sekondari ya Arusha girl
amesema ni Kutokana na kuwepo uhitaji wa taulo hizo hususani Mabinti
wanapokua shuleni Shirika hilo limewiwa kutoa zawadi hizo Kwa wanafunzi
hao.
Hata
hivyo mbali na kutoa zawadi hizo Shirika hilo lilitoa Elimu kwa
Mabinti hao kuhusu Hedhi Salama pamoja na kuvunja upendeleo Ili kuleta
Mabadiliko (Bias) katika Taifa letu na kuhakikisha Kila Binti anafikia
Malengo.
No comments:
Post a Comment