Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip
Mpango akizindua Kamusi Kuu ya Kiswahili Toleo la 3 wakati wa ufunguzi
wa Kongamano la Pili la Idhaa za Kiswahili Duniani, uliofanyika katika
ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Arusha (AICC).
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip
Mpango akizindua kitabu cha Matumizi ya TEHAMA katika Tasnia ya Habari
kilichoandikwa na Victor Elia, Mtumishi wa Shirika la Utangazaji la
Taifa (TBC) wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Pili la Idhaa za
Kiswahili Duniani, uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa
Arusha (AICC).
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip
Mpango akipokea tuzo ya Nishani ya Heshima ya Rais Samia Suluhu Hassan
kwa kuwa mtumiaji mahiri wa lugha ya Kiswahili aliokabidhiwa na Waziri
wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa, wakati wa ufunguzi wa
Kongamano la Pili la Idhaa za Kiswahili Duniani, uliofanyika katika
ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Arusha (AICC)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip
Mpango akipokea tuzo ya Nishani ya Heshima ya kuwa mtumiaji mahiri wa
lugha ya Kiswahili aliokabidhiwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mohamed Mchengerwa, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Pili la
Idhaa za Kiswahili Duniani, uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa
mikutano wa Arusha (AICC).
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip
Mpango akizungumza na washiriki wa Kongamano la Pili la Idhaa za
Kiswahili Duniani, wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo uliofanyika
katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Arusha (AICC) leo tarehe 14
Machi 2022
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip
Mpango leo tarehe 14 Machi 2022 amefungua Kongamano la Pili la Idhaa za
Kiswahili Duniani, ufunguzi uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa
mikutano wa Arusha (AICC).
Makamu
wa Rais amewaasa wataalamu, mabingwa na wapenzi wa lugha ya Kiswahili
kuendelea kuandika vitabu vya taaluma mbalimbali kwa lugha ya Kiswahili
ili kuepusha ongezeko la upotoshaji wa matumizi wa lugha ya Kiswahili
miongoni mwa jamii husasani wanahabari wanaotumia maneno yasiyo rasmi au
kuchanganya kiswahili na maneno ya lugha nyingine.
Amesema
ubunifu unahitajika katika ufundishaji na uwasilishaji wa lugha ya
Kiswahili kwa kutumia teknolojia ya kisasa, ili kuendana na kasi ya
maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA). Aidha amesema
Katika tasnia ya habari, ni muhimu kuwa na vifaa bora vitakavyowezesha
maarifa ya lugha hii yafike popote yanapohitajika kwa haraka na ufasaha.
Makamu
wa Rais ameongeza kwamba Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais
Samia Suluhu Hassan ipo tayari kushirikiana na Taasisi na wadau
mbalimbali katika kusimamia kwa karibu Mkakati wa Taifa wa kubidhaisha
Kiswahili ambao utazinduliwa rasmi siku ya kilele cha maadhimisho ya
Siku ya Kiswahili Duniani na kuhakikisha kuwa unatekelezwa kikamilifu
ili kufikia malengo yaliyokusudiwa. Amesema Serikali itaendelea
kuhamasisha ufundishaji wa Kiswahili kwa wageni kupitia Balozi na
kujenga ushawishi kwa nchi nyingine kuingiza Kiswahili katika mitaala
ili kuendelea kusambaza lugha hiyo.
Awali
akimkaribisha Makamu wa Rais, Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo
Mohamed Mchengerwa amesema wizara itaendelea kuweka mazingira wezeshi
kwa wataalamu wa lugha ya kiswahili ili waweze kutumia fursa mbalimbali
za lugha hiyo kama vile ukalimani, tafsiri, ufundishaji, uhariri na
uandishi wa vitabu na majarida. Ameongeza kwamba wizara imeandaa kanzi
data ili kuwatambua wataalamu wa kiswahili nchini katika ngazi zote.
Kwa
upande wake kaimu katibu mtendaji wa Baraza la Kiswahili Tanzania
(BAKITA) Consolata Mushi amesema Kongamano hilo litasaidia kubadilishana
uzoefu na kupata ufumbuzi wa changamoto zinazowapata wanahabari katika
kutumia Kiswahili katika kazi zao. Amesema uzinduzi wa Kamusi Kuu ya
Kiswahili Toleo la 3 utaongeza ufanisi katika tasnia ya habari kwa idhaa
zinazotumia lugha ya Kiswahili kutokana na uwepo wa maneno zaidi ya mia
moja mapya.
Kongamano
hilo la siku tano linabeba kauli mbiu isemayo Tasnia ya Habari kwa
Maendeleo ya Kiswahili Duniani huku likishirikisha wadau wa Kiswahili na
vyombo vya habari kutoka ndani na nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment