Taarifa zilizotufikia asubuhi hii leo Jumapili Machi 13, 2022 ni kiwanda cha Magodoro cha GSM kilichopo Mikocheni jijini Dar es Salaam kimeungua moto
Dar es Salaam. Moto mkubwa ambao chanzo chake bado hakijajulikana leo Jumapili Machi 13, 2022 umeteketeza kiwanda cha kutengeneza magodoro kinachomilikiwa na Kampuni ya GSM kilichopo eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuzimwa kwa moto huo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Zimamoto Kinondoni, Christina Sungwa amesema wamepokea taarifa ya tukio hilo asubuhi 12:50
"Baada ya kupata taarifa hiyo tulifika haraka eneo la tukio, tukaomba msaada kwa wenzetu wa bandari na kampuni binafsi wanaohusika na shughuli za uzimaji moto", amesema.
Kamanda Sunga amesema hakuna taarifa yeyote ya majeruhi na mpaka sasa bado thamani halisi ya hasara iliyopatikana bado haijajulikana.
Naye, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema moto huo umedhibitiwa na haujaleta madhara makubwa.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Sunday, March 13, 2022
Tags
LOCAL#
Share This
About kilole mzee
LOCAL
Labels:
LOCAL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment