Sababu kuu ya vita kati ya Urusi na Ukraine ni hofu. Urusi inahofia kwamba iwapo Ukraine itakuwa mwanachama wa Nato usalama wake utakuwa hatarini . Wakati huohuo Ukraine inaiogopa Urusi. Kutokana na hofu hiyo, alikuwa anataka uanachama wa Nato na hofu yake mara moja ikabadilika na kuwa ukweli.
Hofu nynegine inazungumziwa kati4kati ya vita vya Ukraine na Urusi - hiyo ndio hofu ya uwezekano wa kuzuka kwa vita ya tatu ya dunia. Ijapokuwa hakuna sababu mwafaka kwa kuwepo kwa hofu hiyo, mataifa tofauti pia yameamua kuongeza uwekezaji katika sekta ya ulinzi kutoikana na hofu hiyo. Mifano ya hivi karibuni ni kati ya Ujerumani na china.
Mataifa hayo yote yana njia moja tu ya kuondoka hofu hiyo ya kuzuka kwa vita vyovyote vikuu - na hiyo ni kupitia silaha.
Urusi yaishambulia Ukraine:Mengi zaidi
- MOJA KWA MOJA:Majeshi ya Urusi yazingira Kyiv na miji mingine-Ukraine inahofia kitakachofuata
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
1.Mataifa haya matano yanamiliki ya silaha zilizoko katika soko duniani
Mwanzo wacha tujifahamishe kuhusu mataifa yanayofanya biashara kubwa ya silaha.
Marekani , Urusi, Ufaransa , Ujerumani na China pamoja yanamiliki asilimia 75 ya silaha zote duniani.
Kwasasa Marekani ndio inayoongoza huku Urusi ikiwa katika nafasi ya pili. Lakini Urusi pia inataka kuongoza katika soko hili.
Marekani inaunga mkono Ukraine katika vita hii kwasbabu wataalam wengi wanavitaja kuwa vita kati ya Marekani na Urusi. Kw sasa , marekani na mataifa mengine mengi ya Ulaya yanaisaidia Ukraine na silaha , ambazo pia zimekuwa zikiitishwa na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky .
Kutokana na hilo, madai pia yanatolewa dhidi ya Mrekani kwamba inataka kuongeza soko lake la silaha kutokana na hofu ya usalama.
2- Mataifa yanayonunua silaha nyingi duniani
Kulingana na ripoti ya 2021 ya Taasisi ya Utafiti wa Amani ya Kimataifa kutoka Stockholm (Sipri) yenye makao yake Uswidi, wanunuzi watano wakubwa wa silaha katika soko hili lenye hofu ni Saudi Arabia, India, Misri, Australia na Uchina
Tukiangalia kwa makini nchi zinazouza na kununua, inafahamika kuwa China ndiyo nchi pekee ambayo jina lake liko katika orodha ya nchi zinazouza silaha nyingi zaidi na nchi zinazonunua silaha nyingi zaidi.
Mtaalamu wa masuala ya ulinzi Rahul Bedi anaeleza sababu ya hili. Kulingana na yeye, "Uchina ina fomula ya zamani iliyojaribiwa. Kwanza inanunua silaha kutoka nchi zingine na kisha 'kuirekebisha', kutengeneza kitu bora zaidi na kuiuza."
Uhandisi wa ukarabati unamaanisha kubomoa silaha na kuurekebisha . Katika mchakato huu, China pia inafanya baadhi ya mabadiliko katika silaha hiyo kulingana na mahitaji yake na kisha kuzitumia au kuziuza. Kwa sababu hii, China pia iko mbele katika orodha ya waagizaji wa silaha na pia katika orodha ya wauzaji.
3- Je ni mataifa gani yanayonunua silaha kutoka kwa Urusi?
Ikiwa unatazama orodha ya wale walionunua silaha kutoka Urusi na Marekani ,utagundua kwamba ni mataifa tofauti kabisa .
Kulingana na ripoti ya hivi punde ya SIPRI, wanunuzi watatu wakubwa wa silaha za Urusi ni - India, China, Algeria. India ni mnunuzi mkubwa wa silaha za Kirusi.
Wataalamu wanaamini kwamba kwa sababu hii India haitaki kujihusisha na uvamizi wa Urusi Ukraine. Urusi inasaidia India kwa silaha na pia uhamisho wa teknolojia. Kwa sababu hiyo India ina uwezo wa kutengeneza vitu vingine katika nchi yake pia.
4- Je ni mataifa gani yanayonunua silaha kutoka kwa Marekani
Miongoni mwa mataifa yanayonunua silaha kutoka kwa Marekani, Saudi Arabia, Australia na Korea Kusini ziko mstari wa mbele katika orodha hii.
Lakini sio kwamba India hainunui silaha kutoka Marekani. Kando na Urusi, India pia inanunua silaha kutoka Marekani, Israel na Ufaransa.
Hivi majuzi, katika sekta ya ulinzi, serikali ya Modi iliibua kauli mbiu ya 'India inayojitegemea'. Kwa sababu hii pia India inataka kupunguza utegemezi wake kwa Urusi katika sekta ya ulinzi.
Hii ndio sababu India haipendelei upande wowote katika vita hivi. Iwapo India itasema kitu kinyume na Urusi au kuunga mkono Ukraine, basi inaweza kusababisha mpasuko katika urafiki kati yake na Marekani . Kwa wakati huu, India haiko katika nafasi ya kuanzisha uadui na Marekani.
5- Ni nini kilichobadilika katika soko la silaha la Urusi na Marekani?
Kauli mbiu ya 'India inayojitegemea' kuhusu sekta ya ulinzi imekuwa na athari kubwa kwa Urusi. Kulingana na ripoti ya SIPRI, soko la silaha la Urusi lilikua pakubwa kati ya 2016-18, lakini likapungua sana mnamo 2019-2020.
Katika hili, punguzo la 53% lilitokana na India. Wakati huu, India pia ilichukua silaha kutoka nchi zingine. Ingawa Urusi sasa inageukia Uchina kuuza silaha, lPunguz hilo halijajalizwa kikamilifu.
Wakati soko la silaha la Marekani limekua kwa asilimia 15 katika miaka kumi iliyopita, la Russia limepungua kwa asilimia 22.
Hata hivyo, Rahul Bedi anasema kuwa picha ya soko la silaha inaweza kubadilika kidogo baada ya vita vya Urusi na Ukraine.
Anasema, "Marekani ina pesa na teknolojia. Kwa sababu hii, ni nambari moja katika soko la silaha. Urusi ina teknolojia ambayo hata Marekani haina.
Uchina
ina pesa na bidhaa ziko tayari, mbali na kuwa na uwezo mkubwa wa
viwanda kufanya hivyo. Ikiwa Urusi na China zinakaribia kuifikia
Marekani, basi ni kwa muda gani utawala wa Marekani katika soko la
silaha utaendelea, haijulikani.
No comments:
Post a Comment