Wadau wa Usafirishaji wa Mabasi
yaendayo kasi (DART) wapewa mafunzo ya utendaji kazi wa Kaizen kuendana
na kasi katika utoaji wa huduma ya usafirishaji kwa jiji la Dar es
Salaam.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mafunzo hayo Mkurugenzi
wa Fedha na Maendeleo ya Biashara wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka
(DART)kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji ,Deus Kasmir amesema wadau wa
usafirishaji wakijua falsafa ya Kaizen kutakuwa hakuna muda wa kupoteza
na matokeo yake kama taasisi itakuwa na mafanikio yanayoendana na utoaji
wa huduma bora.
Amesema kuwa mafunzo hayo ni ya awamu ya pili
ambapo kila mtu katika nafasi yake ameshirikishwa katika kuendana na
falsafa ya Kaizen kufanya kuimarisha mifumo ya utoaji huduma
zinazokwenda na viwango vyake.
Kasmir amesema nchi zilizotekeleza
Falsafa ya Kaizen kwa Taasisi na Kampuni ya Biashara zimepiga hatua
ambapo hata Tanzania tunakwenda kwa kasi na DART ndio sehemu ya kutumia
falsafa hiyo ikiwa ni kuimarisha mifumo ya utendaji ya kuharakisha
huduma zilizo bora.
Amesema kazi ya kutoa huduma kwa wananchi
ndio msingi wa maendeleo ya nchi hivyo ni vyema kila mmoja kusimama
katika kutenda kazi.
Aidha amesema changamoto ambazo ziko katika
sekta hiyo ni fursa za kuendana na kupata utatuzi wenye kuimarisha sekta
ya usafirishaji.
Nae Mhadhiri wa Chuo cha Biashara (CBE)
Dk.Mariam Tambwe amesema kuwa katika biashara kuna mambo mengi kama
sehemu ya kutoa elimu lazima kila mtu ajue nafasi yake.
Kwa
upande wake Mhandisi wa Uendeshaji wa DART na Mratibu Katondo Nambiza
amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu sana kwani yanajenga kuimarisha
huduma.
Mkurugenzi wa Fedha na Maendeleo ya Biashara wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Deus Kasmir akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wadau wa usafirishaji wa DART katika kuendana na Falsafa Kaizen ,jijini Dar es Salaam.
Mhandisi wa Uendeshaji wa DART na Mratibu wa Kaizen Katondo Nambiza akizungumza kuhusiana na mafunzo ya Kaizen katika uboreshaji wa huduma kwa wateja wenye matokeo ,jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri wa Chuo cha Biashara (CBE) Mariam Tambwe akizungumza kuhusiana na umhimu wa mafunzo yatayosaidia kutoa huduma bora ,jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya Mgeni rasmi na wadau wa usafirishaji DART mara baada ya kufunguliwa kwa mafunzo ,jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment