BARAZA
la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza
limeridhia kufukuzwa kazi kwa watumishi 52 ambao wamekutwa na makosa
mbalimbali ya kiutumishi.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Sengerema, Yanga Makaga amesema leo Machi 18, 2022
kuwa watumishi hao wamekutwa na makosa mbalimbali ya kitumishi ikiwemo
kusema uongo na kughushi vyeti.
Makaga
amezitaka idara za elimu ya msingi na sekondari kujitathimini juu ya
utendaji kazi huku akionya tabia ya wakuu wa idara hizo kuwahamisha
wakuu wa shule na walimu wakuu wanaodaiwa kufanya ubadhirifu kwenye
maeneo.
Makaga
ametoa agizo kwa ofisa elimu Sekondari na msingi wa halmashauri hiyo
kuwashusha vyeo walimu wakuu waliobainika kufanya ubadhirifu wa mali za
umma katika vituo vyao vya kazi.
Diwani
wa Kata ya Kasenyi, Triphone Marley amesema hakuna sababu ya watumishi
wanaofanya makosa kwenye maeneo yao kuhamishwa vituo vya kazi.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Binuru Shekidele amesema
atasimamia nidhamu ya watumishi Ili kulinda hadhi yao kukemea maovu
yanayofanywa na baadhi ya watu wa halmashauri hiyo.
No comments:
Post a Comment