A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, October 18, 2021

RUVU YAICHAPA COASTAL UNION

 

246242101_822163641798111_259496404538184657_n%2B%25281%2529

Mwandishi wetu, PWANI | TIMU ya Ruvu leo imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi Coastal Union katika michuano ya ligi kuu Tanzania bara uliopigwa katika Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.

Katika dakika ya 61 Saadat Mohamed aliipatia timu yake ya Ruvu Shooting ushindi wa 1-0 dhidi ya Coastal Union.

Bao ambalo limedumu katika dakika zote 90 za mchezo huo huku Coastal ilitafuta kurudisha bao lakini mbinu zao ziliishia ukingoni.

Hata hivyo kwa ushindi huo, Ruvu Shooting inafikisha pointi sita baada ya mechi tatu za mwanzo kufuatia kufungwa 1-0 na Dodoma Jiji FC Jijini Dodoma na kushinda 1-0 dhidi ya Biashara United mjini Musoma na leo ikicheza nyumbani kwa mara ya kwanza msimu huu.

Huku katika upande wa Coastal sio nzuri kwani tangu ligi kuanza leo wamekamilisha mechi tatu bila ushindi kufuatia sare mbili za nyumbani 1-1 na Azam FC na 0-0 na KMC Uwanja wa Mkwakwani Jijiji Tanga.

Kwa upande wa mchezo mwingine wa ligi kuu leo, Mbeya Kwanza imelazimishwa sare ya 0-0 na Dodoma Jiji Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.

Mbeya Kwanza inafikisha pointi tano baada ya mechi tatu, ikitoka kushinda 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar ugenini na sare nyingine ya 2-2 dhidi ya mahasimu wao wa Jiji, Mbeya City, wakati Dodoma Jiji baada ya kuichapa Ruvu 1-0 nayo ilichapwa 1-0 na Simba nyumbani, Uwanja wa Jamhuri.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages