A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, September 23, 2021

RC MAKALLA AISHUKURU LIONS CLUB KWA MSAADA WA MADAWATI NA MAJI.




- Atoa Miezi mitatu kwa wavamizi wa Shule ya msingi Mzinga B kuondoka.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amepokea msaada wa Madawati 200 kutoka Club ya Lions ya Jijini humo kwaajili ya Wanafunzi wa shule ya Msingi Mzinga B iliyopo Halmashauri ya Jiji la Ilala ambapo ametoa siku 90 kwa wavamizi wa Shule hiyo kuondoka.


RC Makalla ametoa agizo hilo Mara baada ya kupokea Malalamiko kutoka kwa Wanafunzi na Walimu wa shule hiyo Waliolalamikia Ufinyu wa eneo la Shule baada ya zaidi ya Wavamizi 24 kujenga nyumba ndani ya eneo hilo na kusababisha Kukosekana kwa Maeneo ya Kuendeleza Majengo na eneo la michezo ambapo tayari Serikali imeshinda kesi lakini mpaka Sasa wavamizi bado hawajaondoka.


Kutokana na hilo RC Makalla ametoa maamuzi ya busara ya kuwataka Wavamizi hao kuondoka ndani ya siku 90 kuanzia Sasa ili kupisha eneo hilo litumike kwaajili ya Ujenzi wa Vyumba vya madarasa na maeneo ya michezo.


Aidha RC Makalla ametoa maelekezo kwa Halmashauri zote za Mkoa huo kufanya Maoteo ya idadi ya Wanafunzi wanaohitimu na watakaoandikishwa kujiunga darasa la kwanza na kuanza Ujenzi wa madarasa ili kuepuka suala la uhaba wa madarasa.


Hata hivyo RC Makalla amepokea changamoto ya mahitaji ya Vyumba vinne vya madarasa Katika shule hiyo na kuwahakikishia kuwa tayari Halmashauri ya Jiji la Ilala Imetenga fedha kwaajili ya Ujenzi wa Majengo hayo.


Pamoja na hayo RC Makalla ameipongeza Lions club ya Jiji Hilo kwa kutoa mchango huo wa Madawati, meza za walimu, makabati na kuchimba kisima Cha maji shuleni hapo ambapo amewaomba Wadau wengine kuiga mfano huo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages