A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, September 22, 2021

Daktari kuzunguka dunia nzima kwa baiskeli akihamasisha upandaji miti

 



Dk Raj Phanden (Baba wa Baiskeli), ambaye ni mwanaharakati wa mazingira kutoka mji mdogo wa Bhuna, Wilaya ya Fatehabad, India, yuko nchini Tanzania kuhamasisha utunzanji wa mazingira.

Anasema amekuwa daktari wa binadamu kwa takriban muongo mmoja huko Haryana, India. “Nilikuwa na hospitali yangu binafsi kwa miaka 10 mji wa Bhuna. Ilikuwa ikiitwa Aastha. Nilianza mwaka 2016 na dhima ‘Wheels for Green’ (Magurudumu kwa Kijani) kutoka India kwa baiskeli, nikizunguka duniani kuhamasisha kuachana na uchafuzi wa mazingira, kuongezeka kwa joto duniani, mabadiliko ya tabia nchi na madhara yake kwa binadamu na kuwasihi sana watu wapande miti.”

Anasema alianza safari yake kutoka mji wake wa kuzaliwa, Bhuna (Haryana), na amesafiri zaidi ya kilomita 61,000 kwa kipindi cha miaka mitano kwa baiskeli tu. “Mpaka sasa nimesafiri nchi 60 kwa baiskeli.”

Yafuatayo ni majina ya nchi chache ambako ameshafika. Nchi hizo ni Sri Lanka, Bangladesh, Nepal, Bhutan, Maldives, Thailand, Cambodia, Vietnam, Laos na Thailand. Zingine ni Malaysia, Singapore, Brunei, Indonesia, Timor, Brunei, Philippines, Taiwan, Japan, Korea Kusini, Hong Kong, Macau, Oman, UAE, Iran, Azerbaijan, Armenia na Georgia.

Amesafiri pia Uturuki, Italia, Vatikano, San Marino, Slovenia, Croatia, Hungary, Slovakia, Austria, Jamhuri ya Czech, Poland, Lithuania, Latvia, Estonia, Finland, Uingereza, Scotland, Ireland ya Kaskazini na India.

“Kwa sasa niko Tanzania nikiendelea na safari yangu inayoitwa “Cairo hadi Cape Town”. Baada ya kumaliza kusafiri Bara la Afrika, napanga kwenda Amerika ya Kusini na Kaskazini. Lengo langu ni kumaliza kusafiri dunia nzima kwa baiskeli kwa miaka ijayo.”

Anasema kila nchi ambako amefika amepanda miti takriban laki kadhaa kuhamasisha watu wa nchi husika kutunza mazingira kwa kupanda miti. “Aidha, nimekuwa nikiendesha warsha shuleni na vyuoni, nikihamasisha kuitunza dunia yetu.”

Anasema kwa bahati mbaya, mwaka jana kutokana na ugonjwa wa Covid-19, ilibidi aahirishe safari yake na kurudi India. “Kwa sasa, kwa vile hali inaendelea kuwa nzuri zaidi, nimeanza tena safari yangu katika Bara la Afrika kutoka Cairo hadi Cape Town.”

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages