A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, September 17, 2021

Profesa Luhanga afariki dunia

 

1631876912609500-0
Dar es Salaam. Aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Matthew Luhanga amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali moja jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Ijumaa Septemba 17, 2021 Mratibu wa Mawasiliano na Habari wa UDSM, Dk Dotto Kuhenga amethibitisha kutokea kwa kifo hicho Septemba 16 wakati akipatiwa matibabu.

Ni kweli tumempoteza Profesa Luhanga ambaye alikuwa Makamu Mkuu wa Chuo chetu kwa muda mrefu. Siwezi kuzungumzia zaidi kuhusu ugonjwa wake lakini alikuwa amelazwa hospitali,” amesema Dk Kuhenga.

Dk Kuhenga ameeleza wasifu wa Profesa Luhanga akisema aliajiriwa rasmi katika chuo hicho kama mhadhiri mwaka 1978 baada ya kufanya kazi hiyo kwa miaka miwili kama mhadhiri wa muda wakati huo akiwa Afisa elimu.

Amesema mwaka 1982, alipandishwa cheo na kuwa mhadhiri mwandamizi. Mwaka 1986, alipanda na kuwa profesa mshiriki na mwaka 1990 akawa profesa kamili, akiwa ni mmoja kati ya maprofesa wachache nchini waliofikia hatua hiyo.

Mbali na kuwa kiongozi wa chuo, Profesa Luhanga amekuwa mjumbe wa bodi mbalimbali na ameandika machapisho mengi hasa katika sekta aliyobobea ya telecommunication (mawasiliano),” amesema.
20190830_050755_UDSM_Top%2BUniversity%2Bof%2BDar%2Bes%2BSalaam%2BManagement%2Bin%2Ba%2Bsouvenir%2Bphoto%2Bwith%2Bthe%2Bformer%2BVice%2BChancellor%2BProf.%2BMatthew%2BLuhanga%2Bwhen%2Bthey%2Bwent%2Bto%2Bconsole%2Bhim%2Bafter%2Bhe%2Blost%2Bhis%2Bwife.
Menejimenti ya Juu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika picha ya ukumbusho na Makamu Mkuu wa zamani Profesa Matthew Luhanga walipoenda kumfariji baada ya kufiwa na mkewe, tarehe 27th August 2019

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages