A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, September 16, 2021

MWENYEKITI UWT TAIFA APOKEA WANACHAMA 10 KUTOKA CHADEMA MKOANI SINGIDA

 Charles James, Michuzi TV


MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Gaudentia Kabaka amepokea wanachama 10 kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambapo amesema kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya CCM inayoongozwa na Rais Samia Suluhu ndio inawavutia wapinzani kujiunga na chama hicho.

Kabaka amesema uwezo wa Serikali ya CCM kushughulikia matatizo na changamoto za watanzania umekua ukiwavutia wapinzani ambapo amesema idadi kubwa ya wanachama wa vyama vya upinzani kujiunga na CCM itaendelea.

Hayo yamefanyika katika ziara ya Mwenyekiti huyo wa UWT Taifa katika Wilaya za Manyoni na Iramba Mkoani Singida ambapo yeye ni mlezi wa kichama wa Mkoa huo.

Akiwa ziarani humo Kabaka amekagua ujenzi unaoendelea  wa nyumba ya Katibu wa UWT wilaya ya Iramba wenye gharama ya Sh Milioni 34 ambapo amefurahishwa kasi inayoendelea katika ujenzi pamoja na thamani ya fedha inayotumika kujenga huku yeye mwenyewe akichangia kiasi cha Sh Milioni Moja kufanikisha ujenzi huo.

Pia Kabaka amekagua  jengo la lishe lililopo katika hospitali ya Kiomboi wilayani Iramba ambalo limegharimu kiasi cha Sh Milioni 150 ambalo nalo ameridhishwa na kasi ya ujenzi huo.

Mwenyekiti Kabaka pia ametembelea kikundi cha wajasiriamali kiitwacho JIPEMOYO ambacho kinajishughulisha na kilimo Cha Alizeti  chenye ukubwa wa ekari 10 na ufugaji wa nyuki mizinga 45.

Kikundi hiki kimenufaika na mkopo usio na riba ulitolewa na Halmashauri ya wilaya ya Iramba ambapo idadi ya kikundi hiko ni watu 20 na wamekopeshwa  kiasi Cha Shilingi Milioni 10.

Aidha Kabaka amewasihi viongozi wa serikali kuhakikisha wanatumia vizuri fedha zinazotolewa na Serikali katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo.Pia amewakumbusha kuwa makini katika ujenzi wa miradi inayoendana thamani halisi ya Fedha zinazotolewa na Serikali kuu au  zile zinazotokana na makusanyo ya vyanzo vya mapato ya  Halmashauri husika.

Mwenyekiti wa UWT Taifa akishiriki ujenzi wa Nyumba ya Katibu wa Wilaya ya Iramba ambapo pia amechangia kiasi cha Sh Milioni Moja kufanikisha ujenzi huo.

Wanachama wa Umoja wa Wanawake Tanzania Wilaya ya Iramba na baadhi ya wananchi wakimsikiliza Mwenyekiti wa UWT Taifa alipofika kuzungumza nao na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Mwenyekiti wa UWT Taifa, Gaudentia Kabaka akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM katika Wilaya ya Iramba alipofika kukagua miradi ya maendeleo Wilayani humo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT, Gaudentia Kabaka akipokea kadi ya Chadema baada ya mwanachama huyo kuirudisha na kuomba kujiunga na Chama Cha Mapinduzi CCM.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages