A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, September 16, 2021

Katika Hali Isiyokuwa Ya Kawaida, Kesi Ya Ugaidi Inayomkabili Mbowe Na Wenzake Watatu Yashindwa Kuendelea

 

Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe wakwanza kulia akiwa na wenzake watatu wakiwa katika mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi maarufu Mahakama ya Mafisadi jijini Dar es Salaam leo Septemba 16,2021.
Na Karama Kenyunko Michuzi Tv
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na wenzake watatu imeshindwa kuendelea kusikilizwa kwa wakati uliopangwa kufuatia taratibu zilizowekwa na Mahakama ikiwemo kuzuia wafuasi wa Chadema kuingia na simu katika ukumbi wa Mahakama utaratibu ambao unapingwa na mawakili wa utetezi wakiongizwa na wakili, Peter Kibatala.

Kesi hiyo ambayo leo Septemba 16,2021 ilikuwa inakuja kwa ajili ya shahidi wa upande wa Jamuhuri RPC Ramadhani Kingai ambaye ni shahidi wa kwanza katika kesi ya msingi na kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi kuhojiwa na mawakili wa upande wa huo kufuatia upande wa utetezi kumaliza kumuhoji shahidi huyo, (Re Examination) ilipangwa kuanza kusikilizwa aaa nne kamili asubuhi hii, lakini mpaka sasa saa sita kesi hiyo bado haijaanza.

Wakati wadau mbalimbali wa mahakama wa wakiwa wameishaingia kwenye ukumbi wa wazi wa mahakama kwa wakisubiri kesi kuanza kusikilizwa, karani wa mahakama hiyo alitoa tangazo la kuwataka watu wote watoke nje ya ukumbi huo wa wazi na kuwaacha watuhumumiwa ndani.

Hata hivyo muda mfupi baada ya wadau hao kutoka nje, watuhumiwa nao walitolewa na kurudishwa katika mahabusu ya mahakama hiyo.

Mpaka sasa wadau wa mahakama hao wako nje wakisubiri kujua hatma ya usikilizwaji wa kesi hiyo.

Ikumbukwe kuwa, jana septemba 15, 2021 upande wa utetezi ukiongozwa na wakili wao Peter Kibataka kupinga mahakama isipokee maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa pili Adam Kusekwa ambayo yalipaswa kutolewa mahakamani hapo kama kielelezo na shahidi wa kwanza wa upande wa Mashtaka, Kingai. Wakidai kuwa mshtakiwa kabla ya kuchukuliwa maelezo hayo wakati akichukuliwa maelezo aliteswa na pingamizi la pili ni kwamba maelezo hayo yalichukuliwa nje ya muda.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages