A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, September 8, 2021

BENKI YA MWANGA HAKIKA LTD KUFANYA MKUTANO WAKE WA KWANZA WA WANA HISA SEPTEMBA 18,2021

 

 




Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.
Benki ya  Mwanga Hakika Microfinance Limited imesema kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake imeweza kuwafikia wananchi kwa kuongeza idadi ya mawakala zaidi na kufungua matawi mapya nchini.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki hiyo Projest Massawe katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye Ofisi za Benki hiyo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumzia Mkutano Mkuu wa wanahisa wa Benki hiyo unaotarajiwa kufanyika Septemba 18, mwaka huu.

Projest ameeleza kuwa mkakati wa Benki hiyo ni kuwafikia wateja wengi zaidi kwa kutumia njia mbalimbali zikiwemo mawakala ambao mpaka Sasa wapo zaidi ya 50 na kwamba kwa mwaka huu wataongeza mawakala wengi zaidi.

Akizungumzia mkutano mkuu wa wanahisa Massawe amesema kuwa mkutano huo utafanyika Katika Wilaya ya Mwanga Mkoani kilimanjaro na maandalizi yote yamekamilika.

"Benki yetu itakuwa na Mkutano wa kwanza na wanahisa wake ikiwa ni utekelezaji wa Sheria ya Makampuni ambayo inazitaka Kampuni au Taasisi kuwa na mikutano ya Mwaka ya wanahisa ujadili Mambo mbalimbali ya mwenendo wa Taasisi"  amesema Projest.

Aidha ameongeza kuwa mkutano huo utajudhuriwa na watu wachache Katika ukumbi na wengine watakiunga kwa njia za mtandao  'Video Conference', ikiwa ni matokeo ya hatua za kujikinga na ugonjwa wa homa ya mapafu wa Covid-19.

Kufanyika kwa mkutano huo kunatoa fursa kwa wanahisa wa Benki hiyo kuweza kujadili mwenendo wa Benki yao na kuona namna gani watakavyoweza kupata gawio la faida kulingana na watakavyokubaliana.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages