Mkuu wa
Kitengo cha Biashara wa Akiba Commercial
Bank Webster Kaunga (kulia) akikata
utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa benki
hiyo ilipozindua huduma za Akiba Wakala katika Tawi la Makao Makuu barabara ya
Ohio jijini Dar es Salaam jana wengine pichani n Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa
Akiba Commercial Benki PLC (ACB), Dora Siria na
Mkuu wa Kitengo cha mikopo wa Benki hiyo Charles Kamoto.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Akiba
Commercial Bank Dora Saria amesema benki hiyo imeanzisha huduma ya Wakala
ijulikanayo kwa jina la Akiba Wakala.
Huduma hii itawasaidia wateja wa benki hiyo kupata huduma kwa urahisi zaidi
popote pale walipo kupitia mtandao mpana wa huduma za Wakala unaopatikana nchi
nzima.
Dora Saria ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo kwenye tawi la
benki hiyo ililopo baeabaea ya Ohio mkabala nahoteli ya Serena jijini Dar es
salaam jana.
Amesema Mteja anaweza kupata huduma ya kutoa na kuweka fedha mahali popote
penye tangazo la Akiba Wakala Kupitia huduma hii tutawafikia Watanzania wengi
popote pale walipo na wataweza kunufaika na huduma zetu.
Pia ameongeza kuwa kwamba, kupitia huduma hii ya Akiba Wakala Benki watakuwa
washiriki wazuri katika kuunga mkono harakati za Serikali za kuhakikisha uwepo
wa huduma jumuishi za kifedha yaani (Financial inclusion) kwa Watanzania wote.
Tumeingia sokoni na jumla ya Wakala wapatao 200 na lengo letu ni kuendelea
kuongeza Wakala wengi kadri iwezekanavyo kwa lengo la kukidhi kiu ya upatikana
wa huduma za Akiba nchi nzima, kwa urahisi na ukaribu kwa kumfata mteja popote
alipo au kwa urahisi waweza kusema pasipo na ulazima kwa kufika tawini.
Aidha, Benki itaendelea kuboresha huduma hizi za Akiba Wakala kwa kuhakikisha
upatikana wa mahitaji mengi ya kibenki kadri iwezekanavyo kwa Wakala wetu kwa
lengo la kuleta urahisi na huduma zaidi kwa wananchi kama tulivyoainisha kwenye
kauli mbiu ya huduma hii ya Akiba Wakala ambayo inasema Huduma Zaidi.
“Tunategemea kutoa huduma za kufungua akaunti na nyinginezo nyingi hapo
mbeleni. Vile vile Benki imeanzisha mkakati rasmi wa kuhakikisha kuingia rasmi
katika mfumo wa kidigitali katika mchakato wa kutoa huduma.”. Amesema Dora
Saria
Mfumo huu utaendelea kuleta unafuu na kuokoa gharama za upatikananji wa huduma
zetu.Pia tunazo huduma za Akiba Mobile, ambazo zinawawezesha wateja wetu kupata
mahitaji mbali mbali ya Kibenki na mengineyo mathalani kununua LUKU,
ving’amuzi, muda wa maongezi pamoja na malipo yote ya Serikali kupitia simu zao
za mikononi.
Ameongeza kuwa wateja wote wa Benki ya Akiba wanaomiliki akaunti binafsi
wanakuwa wameunganishwa na huduma hii na wanaweza kufanya miamala popote pale
walipo. Huduma ya Akiba Mobile inaptikana kupitia mfumo wa USSD na App kwa wale
wanoatumia simu janja.
Pia huduma ya Akiba Mobile inamuwezesha mteja kufanya miamala yake ya kibenki
kupitia Akiba Wakala vile vile.Kabla ya hitimisho naomba pia niwadokeze ndugu
wnahabari kuwa Benki ya Akiba inatoa huduma nyingine nyingi za Amana, Mikopo,
kuuza na kununua float, kutuma na kupokea fedha kupitia Western Union n.k.
Ametoa rai kwa Watanzania wote watembelee matawi yetu yote pamoja na Akiba
Wakala kwa ajili ya kuhudumiwa na ufafanuzi.Kwa kumalizia, ikumbukwe kwamba
benki yetu imepata mwekezaji wa kimkakati, ambaye ni National Bank of Malawi
(NBM).
Ni imani yetu kwamba ubia huu utasaidia kupanua wigo wetu wa kibiashara
ikizingatiwa NBM ni moja ya benki kubwa kwenye ukanda wetu wa nchi kusini mwa
Afrika.
Vile vile, tutaendelea kuboresha na kuanzisha huduma nyingi zikiwemo za kidijitali na hizi za Akiba Wakala imezinduliwa rasmi na tunawakaribisha Wateja wetu wote watumie huduma hiyo kwa mahitaji yako kibenki na wakumbuke kuwa hawana ulazima wa kufika matawini kwa ajili ya kuweka na kutoa fedha kwenye Akaunti zao, kufanya marejesho ya mikopo
No comments:
Post a Comment