Wananchi
wakiwa katika banda la JATU PLC wakipata maelezo kabla ya kununua hisa
za kampuni hiyo.JATU wapo katika maonesho ya 45 ya biashara ya kimaifa
yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere maarufu Sabasaba wilayani
Temeke mkoani Dar es Salaam.
Maofisa
wa Kampuni ya JATU PLC wakimhudumia mmoja ya wananchi aliyefika kwenye
banda lao kwa ajili ya kununua hisa za kampuni hiyo.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam | KAMPUNI
ya JATU PLC imewaomba wananchi wanaotembelea Maonesho ya 45 ya Biashara
ya Kimataifa kutembelea banda la kampuni hiyo ili kupata taarifa
mbalimbali zinazohusu namna ya wananchi kujikomboa kiuchumi kupitia
kauli mbiu inayosema Buku Tano inatosha.
Akizungumza
na Michuzi Blog na Michuzi TV Ofisa Masoko wa Kampuni ya JATU PLC
Ngorosho Winfrida amesema huu ni wakati muafaka wananchi wanaokwenda
kutembelea maonesho hayo wakafika banda la JATU na wakiwa hapo watapewa
maelezo ya umuhimu wa kununua hisa ili kubadilisha maisha yao kiuchumi.
Amefafanua
kwamba JATU PLC wapo kwenye viwanja vya Sabasaba yanakoendelea maonesho
hayo na kazi wanayoendea nayo ni kuhamasisha wananchi kununua hisa na
kauli yao ni Buku tano inatosha na kiasi hicho cha fedha kinatosha
kumfanya mwananchi kununua hisa.
Ameongeza "Tunaomba
wananchi wafike kwenye banda la JATU PLC, tuko kwa ajili yao na kwa
wale ambao watanunua hiisa zetu watapata fursa ya kujikomboa kiuchumi
kwani baada ya kununua hisa tutawapa fursa za kushiriki kikamilifu
katika shughuli za kujikomboa kiuchumi kupitia kilimo na shughuli
nyingine zitokanazo na kilimo pamoja na nafaka."
"JATU
tupo kwenye viwanja hivi vya Mwalimu Nyerere Sabasaba na kubwa zaidi
tumekuja na kauli mbiu yetu ya Buku tano inatosha ambapo fedha hiyo
itamwezesha mwananchi kununua Hisa."
Aidha
Ngorosho amesema kampuni hiyo ni Mtanzania na lengo lake kubwa ni
kushirikiana na jamii ya Watanzania kupata fursa ya kushiriki katika
shughuliza kiuchumi na hatimaye kujikomboa kiuchumi,na kubwa zaidi
amedhamiria kufanya mageuzi katika sekta ya kilimo.
Pia
Ngorosho amesema kwa sasa wapo hatua za mwisho kwani kampeni yao
inayosema Buku Tano inatosha inatarajia kumalizika mwishoni mwa Julai,
2021, hivyo ni vema wakachangamkia kununua hisa za kampuni hiyo hasa
katika siku zilizobakia.
"JATU
PLC licha ya mambo ya hisa lakini imejikita kwenye kilimo ambapo
tunajihusisha na shughuli za kilimo katika maeneo karibu yote nchini
Tanzania, lakini tunayo masoko kwa ajili ya bidhaa za nafaka ambayo yapo
ndani na nje ya Tanzania, hivyo tunayo masoko ya uhakika a ukiwa na
hisa za kampuni yetu mwana hisa anayo nafasi ya kuchagua anataka
kujikita kwenye eneo gani," amesema Ngorosho.
No comments:
Post a Comment