A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, June 24, 2021

ZAMBIA YATANGAZA RATIBA YA MAZISHI YA HAYATI DK. KENNETH KAUNDA, MWILI KUZUNGUSHWA MIKOA 10

 

cxxinwo0lry66fifasb7

LUSAKA, Zambia | SERIKALI ya Zambia imetangaza ratiba ya mazishi ya mwili wa mwasisi wa taifa hilo, Dk. Kenneth Kaunda, aliyefariki dunia Juni 17, mwaka huu.

Makamu wa Rais wa nchi hiyo, Inonge Wina, amesema ratiba hiyo inaanza leo, Juni 23, mwaka huu kwa mwili kuzungushwa katika mikoa 10 ili kuwapa fursa wananchi kutoa heshima zao za mwisho.

Amesema wakati mwili huo ukiagwa, taifa litaendelea kuwa katika maombolezo ya siku 21 na kituo cha taifa cha televisheni kitarusha moja kwa moja matukio yote.

Makamu huyo wa Rais wa Zambia, amesema msafara wa mwili wa Kaunda utapita katika makao makuu ya mikoa pekee.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages