A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, June 24, 2021

RC MAKALLA AWAPONGEZA NMB KWA KUTOA MIKOPO KWA WATUMISHI

 

WhatsApp%2BImage%2B2021-06-23%2Bat%2B2.38.53%2BPM

Awapa Somo la "MSHAHARA WAKO NI SAWASAWA NA MATUMIZI NA KUJIWEKEA AKIBA"

(Income = Consumption + Savings).

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amewataka Watumishi kukopa kwa malengo ya kuboresha maisha ya Sasa na baadae na kuhakikisha mikopo wanayochukuwa wanaitumia kuanzisha miradi yenye tija.

WhatsApp%2BImage%2B2021-06-23%2Bat%2B2.38.55%2BPM

RC Makalla amewataka Walimu kuacha kurubuniwa kwa mikopo ya Chapu Chapu yenye riba kubwa ambayo mwisho wa siku inawaingiza Katika Maisha Magumu badala ya neema.

Aidha RC Makalla amewapatia Walimu somo la namna Bora ya kutumia Mshahara wao na kuweka akiba kwaajili ya kuanzisha miradi ya kujiimarisha kiuchumi ili watakapostaafu Waweze kuishi maisha Bora.

Hayo yote yamejiri wakati wa ufunguzi wa Semina ya Siku ya Walimu iliyoandaliwa na bank ya NMB.

WhatsApp%2BImage%2B2021-06-23%2Bat%2B2.38.54%2BPM
Picha ya Pamoja

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages