A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, May 13, 2021

TAHA YAWAPIGA TAFU WANA KONGANI YA ZAO LA PARACHICHI WILAYANI ARUMERU

Asasi ya kilele ya sekta binafsi inayojishughulisha na kilimo cha horticulture yaani mboga, matunda na mimea itokanayo na mizizi pamoja na viungo(TAHA) imezindua kongani ya zao la Parachichi kanda ya Kaskazini katika kijiji cha Ngyani kata ya Nkoaranga halmashauri ya Meru wilayani Arumeru mkoani Arusha kwa kuhamasisha uwekezaji katika zao hilo kutokana na fursa kubwa ya masoko iliyopo katika soko la kimataifa.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa kongani hilo mkurugenzi mtendaji wa asasi hiyo Dkt Jackline Mkindi alisema kuwa wameamua wanahamasisha wananchi kulima zao hili kwakuwa linaitajika sana Katika nchi za nje pia litasaidia kuwanufaisha wananchi na kuowaondoa Katika umaskini pia litasaidia kujenga uchumi wa nchi.

Alisema mpaka kongani hiyo ya parachichi ina jumla ya wakulima wadogo 200 lakini bado wengine wakaendelea kujiunga ambapo alifafanua kuwa wananchi hao tayari wametenga hekari 250 kwa ajili ya kilimo hicho cha parachichi.

"Na katika kwenda mbali zaidi wakulima hawa wadogo wameweza kununua miche ya kisasa ya miparachichi 500 na sisi Kama TAHA tumeweza kuwaongezea mingine 500 pia wataalam wetu wataendelea kuwapa elimu ya kilimo hichi na kuwafatilia hadi pale watakapo anza kuvuna ambapo pia tutawatafutia masoko ya nje maana ndipo kunauhitaji mkubwa sana "alisema Mkindi.

 Alibainisha kuwa kwa mwaka uliopita uzalishaji wa zao hilo ulikuwa ni tani 39,000 huku uuzaji nje ya nchi ukiwa ni tani 8500 hadi 9000 ambayo iliingiza dola za kimarekani milioni 30 ambapo kwa miaka mitatu ijayo kutokana na uwekezaji zao hilo wanatarajiwa kuingiza zaidi ya bilioni 22 kutokana na uhitaji mkubwa uliopo katika soko la kimataifa.

“Katika zao hili la Parachichi uzalishaji katika shamba lenye ukubwa wa hekari moja ni tani 2.7 hadi tani 7 ambapo faida yake kama mtu atauza katika soko la kimataifa atapata shilingi milioni 4 hadi milioni 4.5 kwa hekari moja lakini pia zao hili linaongeza uzalishaji kadri mti unapoongeza miaka na kuzalisha tani 8 hadi kumi ambayo faida yake ni milioni 13 na kama mtu ana hekari nyingi zaidi atapata zaidi,”Alisema Dkt Jackline. 

Alifafanua kuwa katika shamba la hekari moja inaweza kuoteshwa miti 120 na gharama ya kuwekeza ni shilingi milioni 1.1 huku gharama ya kuhudumia shamba ikiwa sio zaidi ya shilingi laki tano ambapo TAHA wanaendelea kuwajengea uwezo wakulima juu ya zao hilo pamoja na kuhakikisha kuwa wanazalisha mazao yenye ubora unaohitajika katika soko la kimataifa.

Aidha aliendelea kusema kuwa serikali imewaongezea ufanisi mkubwa wa kuyafikia masoko kwa kuboresha miundombinu ya usafiri ambapo wanasafirisha mazao kwa kupitia nji ya anga na maji na hadi hivi sasa wanauwezo wa kupeleka mazao hayo katika nchi 198 duniani.

Alieleza kuwa zao hilo linafursa nyingi ikiwemo kutunza mazingira, ni tunda, linakamuliwa mafuta pamoja na kokwa lake kutengenezewa bidhaa za kutunza ngozi hivyo ifike mahali wakulima wawekeze katika zao hilo ka wingi kwani linachangia katika ukuaji wa uchumi.

Kwa upande wake msaidizi wa katibu tawala mkoa wa Arusha Agney Chitukuro akimwakilisha kaimu katibu tawala mkoa wa Arusha David Lymongi alisema kuwa kama serikali wanafahamu kazi nzuri wanayoifanya TAHA ambapo mkoa kupitia halmashauri zake watashirikiana nao pamoja na kuhakikisha uwekezaji wa zao hilo unafanikiwa kwa asilimia kubwa.

Alisema tasnia ya horticulture imetoa ajira kwa akina mama wengi na vijana na ni fahari ya serikali kuoa kuwa pato la parachichi linapanda kila mwaka ambapo aliwataka wanachi kuchangamkia fursa hiyo kwani ipo na tayari wana uhakika wa masoko.

“ Ni vizuri mnunuzi anapokuja anapata mzigo wa kutosha katika eneo moja hivyo tumieni fursa hii kwani ni uwekezaji wenye faida kubwa na ni wa muda mrefu takriban miaka 40 na nyie Taha nihakikishie kuwa uongozi wamkoa utato ushirikiano wa kutosha ili wakulima waweze kupata faida na kuinua uchumi wao,” Alisema Chitukuro

Diwani wa kata ya Nsongoro Kaanaeli Ayo aliishukuru TAHA kwa kwa kuwapelekea fursa hiyo na wanaamini kuwa uchumi wao utaenda kuimarika kwani awali walikuwa wanategemea zao la Kahawa ambalo kwa sasa wameshindwa kuendelea nayo kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo kushuka kwa uzalishaji.

Nao baadhi ya wanakikundi wa kongani hiyo walisema kuwa baada ya Taha kuwaeleza juu ya fursa zilizopo katika zao la Parachichi wamechukua sehemu kubwa kubadili mazao waliyokuwa wakilima ambayo pia waliyarithi kutoka kwa wazazi wao kama zao la kahawa kwani wapokea kwa nguvu kubwa na wanatarajia kunufaika kwa asilimia 100.

Esta Mungure alieleza kuwa wamekuwa na miti ya parachichi ya kienyeji kwa kiasi kidogo lakini pia haikuwa kwaajili ya biashara hivi sasa wanaingia katika kilimo biashara ya zao hilo kwa kupanda miche ya kisasa waliyoletewa ambayo uzalishaji wake ni mkubwa na utawainua kiuchumi wananchi wengi .
msaidizi wa katibu tawala mkoa wa Arusha Agney Chitukuro akimwakilisha kaimu katibu tawala mkoa wa Arusha David Lymongi akiongea katika uzinduzi wa  kongani ya zao la Parachichi kanda ya Kaskazini katika kijiji cha  Ngyani  kata ya Nkoaranga halmashauri ya Meru wilayani Arumeru mkoani Arusha hivi karibuni (picha na Woinde Shizza ARUSHA).

Mkurugenzi wa asasi ya kilele inayojishughulisha na kilimo cha horticulture yaani mboga, matunda na mimea itokanayo na mizizi pamoja na viungo(TAHA) Jackline Mkindi akipanda mti  Kama ishara ya ufunguzi rasmi wa kongani ya kilimo  cha Parachichi kwa mikoa ya kanda ya kaskazini, uzinduzi uliofanyika Katika viwanja vya chama cha ushirika Ngyani Katika kijiji cha Ngyani vilivyopo kata ya Nkwaranga wilayani Arumeru
 baadhi ya Miche ya parachichi  iliyotolewa na Taha kwa wanakongani hao
Mkuu wa idara ya uzalishaji kutoka Asasi ya kilele inayojishughulisha na kilimo cha Horticulture yaani mboga, matunda na mimea itokanayo na mizizi pamoja na viungo(TAHA) akiwaelikeza mgeni rasmi wa uzinduzi wa kongani ya parachichi ambaye ni kaimu katibu tawala mkoa wa Arusha kushoto Agney Chitukuro pamoja na mkurugenzi wa TAHA Jackline Mkindi kulia namna ya kupanda Miche ya miparachichi zoezi lililofanyika Katika kata ya Nkwaranga wilayani Arumeru mkoani Arusha 
mtaalam kampuni binafsi inayojishughulisha na upimaji wa udongo kwa wakulima wakubwa, wakati na wadogo (LSSL )Haji Salim akiwapa elimu ya faida za upimaji wa udongo kabla ya kulima zao lolote wakulima wa kata ya Nsongoro Wilayani Arumeru Mkoani Arusha juzi (picha na Woinde Shizza , ARUSHA)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages