(Johannesburg, 21 Aprili 2021) Kampuni ya teknolojia ya kimataifa, Huawei inaamini kuwa teknolojia ya
habari na mawasiliano au TEHAMA, ina uwezo wa kupunguza uzalishaji wa kaboni
ulimwenguni kwa asilimia 20 katika muongo mmoja ujao.
William Xu, ni Mkurugenzi
wa Bodi na Rais wa Taasisi ya Utafiti wa Mikakati wa Huawei, hivi karibuni
alisema uendelevu wa nishati ni changamoto kubwa ambayo itazikabili nchi zote
kwa muongo mmoja ujao.
“Matumizi ya nishati
ulimwenguni yanaongezeka kwa kiwango cha asilimia 1.7 kila mwaka. Hivi sasa
asilimia 85 ya nishati hutokana mabaki ya mimea na wanyama wa kihistoria yaani ”fossils”. Uendelevu wa nishati hii ni changamoto kubwa
inayotukabili sisi sote. Kwa kuwezesha sekta mbalimbali, teknolojia ya TEHAMA
ina uwezo wa kupunguza uzalishaji wa kaboni ulimwenguni kwa asilimia 20 katika
muongo mmoja ujao." Xu alisema.
Aliongeza kuwa wakati
nchi nyingi zimejikita kupunguza uzalishaji wa kaboni, mahitaji ya nishati
mbadala yameongezeka, na hapa ndipo TEHAMA inapotoa fursa mpya katika uzalishaji,
uhifadhi na matumizi ya umeme.
"Kwa matumizi ya
nishati, lazima tupendekeze mifumo jumuishi ya nishati kwa majumbani na
viwandani na kuunda jamii, vyuo na miji isiyozalisha kaboni.” alisema Xu.
Hivi karibuni, Huawei
ilitangaza kuwa itazingatia ubunifu na teknolojia mpya kusaidia viwanda
kupunguza matumizi yao ya nishati ili kupunguza uzalishaji wa kaboni
ulimwenguni.
Barani Afrika pia,
nchi nyingi zinazidi kuhamia katika matumizi ya nishati mbadala ili kusonga
mbele katika nishati endelevu kwa siku zijazo.
Pamoja na algorithm
yake ya muunganisho wa gridi inayoendeshwa na utashi wa kutengenezwa
(Artificial Intelligence), Huawei imetoa zaidi ya mifano ya gridi 200 ya umeme
kwa nchi zaidi ya 30. Hii imesaidia mitambo ya umeme kuunganishwa na gridi kwa
uimara huku ikipelekea kuwepo na chanzo bora cha umeme wa jua.
Katika umeme wa jua
pekee, Afrika imepata maendeleo makubwa katika miaka ya hivi karibuni. Zaidi ya
gridi 6,200 ambazo hujumuisha gridi kubwa kabisa, za biashara na viwanda pamoja
na zile ndogo zimethibitishwa kuwepo barani humo.
Kwa kuongezea, mataifa
mengine tisa ya Kiafrika, mbali na Afrika Kusini na Misri, yapo njiani kujiunga
na 'Gigawatt Club', lebo isiyo rasmi kwa kundi la nchi zilizo na uwezo wa
kuzalisha gigawatt moja ya umeme kutokana na jua.
Huang Su, Mkurugenzi
wa Huawei katika Biashara ya Umeme Dijitali Kusini mwa Africa, alisema kwamba
karibu nusu ya idadi ya watu wasio na uwezo wa kupata umeme duniani wanaishi
kusini mwa jangwa la Sahara.
"Kwa hivyo kuna
haja kubwa na ya dharura ya kuharakisha ukuaji wa nishati mbadala kote katika
eneo hilo ili kuhakikisha nishati ya kutosha, nafuu na ya kuaminika kwa
Waafrika wote na kwa nchi kupata faida ya uchumi wa kijani." anasema.
Huawei imetumia zaidi
ya miaka 30 ya utaalam na uzoefu katika teknolojia ya kidijitali ili kufanya
uzalishaji wa umeme wa jua na matumizi kuwa bora zaidi na ya kuaminika kwa
gharama ndogo.
No comments:
Post a Comment