Na Charles James | Dodoma | KUELEKEA
Siku ya Wanawake Duniani ambayo hufanyika kila Mwaka Machi 8, Katibu wa
Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Dodoma Mjini, Diana Madukwa
amesema umoja huo utaendelea kuwaandaa wasichana na wanawake ili kushika
nafasi mbalimbali za kiuongozi.
Madukwa
pia amempongeza Rais Dk John Magufuli kwa namna ambavyo ameendelea
kuwaamini wanawake katika nafasi mbalimbali kubwa za kiuongozi na
kimaamuzi kwenye Serikali yake ikiwemo kuwa na Makamu wa Rais wa kwanza
Mwanamke tokea historia ya Tanzania.
Amesema
UWT Wilaya ya Dodoma Mjini imekua ikiandaa Mafunzo na semina mbalimbali
za kuwajengea wanawake na wasichana uwezo wa kujiamini kwamba wao
wanaweza na siyo lazima awepo mtu mwingine wa kuwasukuma.
"Sisi
kama UWT Wilaya mara kwa mara tunaandaa mafunzo na lengo lake ni
kuwaambia wanawake na wasichana kutokukaa nyuma na kusubiri kufanyiwa
maamuzi, wajiamini na kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za kiuongozi
kuanzia kwenye Chama na sehemu nyingine."
"Mafunzo
yetu yamekua yakijikita zaidi katika kuwajengea uwezo wa kupata uongozi
bila kutoa rushwa ikiwemo ya Ngono, tunawajengea uwezo wa kuongoza,
uwezo wa kujiendesha kiuchumi, kisiasa na kijamii," Amesema Diana Madukwa.
Amempongeza
Rais Dk Magufuli kwa kuendelea kuwaamini wanawake katika nafasi
mbalimbali kwenye serikali jambo ambalo limetoa ari na motisha kwa
wasichana wengi zaidi kujikita kwenye siasa na kuona inawezekana kuwa
sehemu ya uongozi wa Nchi yao.
"Nimpongeze
na kumshukuru sana Rais wetu Dk Magufuli ameendelea kuwaamini wanawake
kwenye nafasi kubwa na nyeti, pamoja na kuwa na Makamu wa Rais Mwanamke
ambaye ni Mama Samia Suluhu Hassan pia tumeona idadi kubwa tu ya
Mawaziri Wanawake, Wakuu wa Mikoa Wanawake na hata kwenye Majeshi yetu,
tumeona Mkuu wa Idara ya Uhamiaji pia ni Mwanamke, tumpongeze Rais kwa
hilo," Amesema Diana Madukwa.
Amesema
UWT Wilaya ya Dodoma itaendelea kutoa elimu na mafunzo ya kuwawezesha
wanawake kujiamini zaidi na kuingia kwenye ushindani wa nafasi za
kiuongozi.
No comments:
Post a Comment