
Katibu
Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya akiwa pamoja na Mkurugenzi wa
Mafunzo na Utafiti Dkt. Wilhelm Mafuru wakati wa kikao hicho na Wadau wa
tasnia ya sukari leo tarehe 5 Machi, 2021 katika ofisi za Wizara ya
Kilimo Jijini Dodoma.

Mkurugeni
wa Bodi ya Sukari Profesa Kenneth Bengesi akichangia mada kwenye
mkutano wa Wadau wa tasnia ya sukari pembeni yake kushoto ni Katibu
Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Tasnia ya Sukari (SIDTF) dkt. Nephat
Mkula leo tarehe 5 Machi, 2021 katika ofiisi za Wizara ya Kilimo Jijini
Dodoma.

Wadau
wa tasnia ya sukari kuanzia kulia ni Mwakilishi wa Wakulima wadogo wa
miwa nchini Balozi Ahmadah Ngemela kutoka Missenyi mkoani Kagera, Guy
Williams Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha sukari cha Kilombero na mwisho
ni Degratias Lyatto Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa
Maendeleo ya Tasnia ya Sukari.

Gere Mlingwa Balozi Mstaafu na Mkulima mkubwa wa miwa akichangia mada katika mkutano huo wa Wadau wa tasnia ya sukari.

Katibu
Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa
kikao hicho cha Wadau akiongoza kikao hicho leo tarehe 5 Machi, 2021
katika ofisi za Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Kilimo mwenye suti ya kijivu katikati akiwa pamoja na Wadau wa tasnia ya sukari baada ya kumalizika kwa mkutano wao.
Katika
kuhakikisha nchi inajitosheleza kwa sukari; Mfuko wa Maendeleo wa
Tasnia ya Sukari (SIDTF) umeidhinisha jumla ya shilingi bilioni 1.6 kwa
ajili ya kugharamia huduma za mafunzo, uendeshaji wa shughuli za Chuo
cha Taifa cha Sukari pamoja na ununuzi wa vifaa vya mafunzo na ukarabati
wa majengo.
Kauli
hiyo ilitolewa na Katibu Mkuu; Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya wakati
wa kikao chake na Wadau wa tasnia ya sukari ikiwemo Bodi ya Sukari,
Wizara ya Kilimo, Wakulima wakubwa na wadogo wa miwa na Wazalishaji
sukari katika ukumbi wa mikutano wa Wizara, Jijini Dodoma leo tarehe 5
Machi, 2021.
Katibu
Mkuu Kusaya amesema ukosefu wa Wakufunzi, uchakavu wa vitendea kazi vya
kuendesha mafunzo na kuchakaa kwa miundombinu ya Chuo cha Taifa cha
Sukari (National Sugarcane Institute – NSI) kulisababisha kusimama kwa
utoaji wa mafunzo ya kilimo cha miwa na uzalishaji sukari kwa muda
mrefu.
Katibu
Mkuu Kusaya amesema kuwa juhudi za Serikali na Wadau wa tasnia ya
sukari za kuimarisha Chuo cha Taifa cha Sukari zimeshaanza na kwamba
zinaendelea kufanyika ili Chuo hicho kiwe bora na kinachotoa mafunzo ya
kilimo cha miwa na uzalishaji sukari nchini.
“Chuo
cha Taifa cha Sukari nchini ndiyo Chuo pekee cha Afrika Mashariki na
Kati kitakachokuwa kikiandaa Wataalam wa teknolojia ya sukari na
kinatariwa kurejea katika kutoa mafunzo Mwezi Septemba 2021 na tutarajie
mabadiliko makubwa.” Amesisitiza Katibu Mkuu Kusaya.
Katibu
Mkuu Kusaya ameongeza kuwa juhudi za Serikali na Wadau zimewezesha Chuo
cha Taifa cha Sukari kupata kibali cha Baraza la Taifa la Elimu ya
Ufundi (NACTE) ili kutoa mafunzo kwa Ngazi ya Astashahada na Shahada ya
kilimo cha miwa (Sugarcane technology) na uzalishaji wa sukari (Sugar
technology).
Naye
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Sukari Bwana Aloyce Kazimili amesema kwa
sasa tayari kuna Walimu ambao wanatoa mafunzo hayo lakini hawakusomea
taaluma ya kilimo cha miwa kwa sababu hiyo Walimu hao ni vyema
wakasomeshwa na Serikali kwenye eneo hilo ili rahisi wao kuajiriwa mara
kibali cha ajira kitakapotolewa.
Katibu
Mkuu Kusaya amemuagiza Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Wizara
ya Kilimo kuwapa uhamisho wa muda Watumishi wawili wa Kitengo cha Ugavi
na Manunuzi na Mkaguzi wa Ndani ili irahisishe hatua za awali za
kuhuisha uanzishwaji wa Chuo cha Taifa cha Sukari pamoja na mambo
mengine amewahidi Wadau wa mkutano huo kuwa atahakikisha ukarabati
unaanza mara moja kwa kutumia Wataalam wa ndani na kwa mvumo wa “force
account”.
No comments:
Post a Comment